PICHA: Watu 29 wapoteza maisha katika ajali ya mabasi ya City Boy, Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi

Ajali mbaya imeyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya City Boy imetokea katika kijiji cha Maweni wilaya ya Manyoni, Singida na kusababisha watu 29 kupoteza maisha papo hapo huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni mwendo kasi.

Mabasi hayo yenye namba za usajili T531 DCE na T247 DCD, moja lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama na lingine likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam.

Moja ya mashuhuda wa ajali hiyo amesema kuwa madereva wa mabasi yote walikuwa katika mwendo kasi na wakati ajali inatokea walikuwa wakisalimiana kwa kunyosheana mikono kisha basi moja kupoteza mwelekeo na kuingia upande wa basi lingine na ndipo yakakutana uso kwa uso na kusababisha ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sedoyeka tayari amethibittisha kutokea ajali hiyo na uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kueleza kuwa amepokea taarifa hiyo kwa mshtuko na amesikitishwa na ajali hiyo ambayo imechukua maisha ya watanzania.



Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. pOLENI NDUGU NA jAMAA WOTE MLIOPATA MSIBA NA KWA TAIFA LETU KUWAPOTEZA FAMILIA NA VIZAZI . MUNGU AKUPENI UJASIRI KATIKA WAKATI HUU MGUMU NA TUNAMUOMBA MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA. AMIN

    ReplyDelete
  2. Hizi ajali au ni mali za freemason zinakula roho za watu wasio na hatia. R.I.P na poleni Sana wafiwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad