Polisi Wakanusha Kuzuia Mikutano ya Kisiasa Tanzania


Jeshi la polisi nchini Tanzania limetoa ufafanuzi kuwa halijazuia mikutano ya vyama vya kisiasa
Katika taarifa yake,limesema kuwa kile lilichozuia ni mikutano ya hadhara ambayo lilihisi itavuruga hali ya usalama

Hivyobasi jeshi hilo sasa limewataka wananchi kupuuza taarifa kuwa wao walizuia mikutano ya kisiasa.

"Jeshi la Polisi linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya kiusalama itakapotengemaa."

Kulingana na nukuu hiyo jeshi hilo linasema kuwa hakuna sehemu yoyote iliyopiga marufuku mikutano ya kiutendaji na kiutawala ya vyama vya kisiasa inayofanywa kwa mujibu wa katiba na kanuni za vyama husika.

Jeshi hilo limetoa mfano wa Chama cha CUF kilichotangaza kuwa kimepanga kufanya mkutano mkuu kujaza nafasi ya Mwenyekiti wao wa Taifa tarehe 21 Agosti, 2016,na ambao Polisi hawakujitokeza kuuzuia.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hmmm.
    Hiyo yote kulinda mkutano wa CCM. Kauli ilitolewa na wote tulisikia na vitebdo tumevishuhudia wenyewe. Hii bandika bandua au kukimbilia kutoa kauli bila kufikiria CCM pia itafanya mikutano.
    Uongozi wa awamu ya tano kutaka kuiimarisha na kuiokoa CCM wakati miaka kumi imepeleka nchi njua panda inakazi.

    ReplyDelete
  2. Mdau taarifa ilikuwa wazi tangu mwanzo mkutano ya hadhara ndio iliyozuiliwa na si mikutano ya ndani ya vyama.nadhani mh lowassa umeongea vizur kabisa na mwenyekiti katoa tamko.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad