Mwenyekiti wa TLP Dkt. Augustino Lyatonga Mrema amesema Rais Dkt. John Magufuli anaishi kwenye maneno yake kwa kuwa mwaka jana alipofika kwenye jimbo la Vunjo aliwaambia wananchi wamchague Mrema na wasipomchagua atampa kazi, jambo ambalo ametimiza
Mrema ameyasema hayo alipofanya mahojiano maalum na EATV kuhusu uwezo wake wa kusimamia Bodi ya Parole ambayo yeye ndiye mwenyekiti wake baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli.
''Nafasi ambayo amenipa Rais Dkt. Magufuli nina uzoefu nayo kwa kuwa mwaka 1994 njia tuliyokuwa tunaitumia ni kutembelea magereza na kuongea na wafungwa hasa wanaotumia vyombo vya moto na wengine walikuwa wanataja walipoficha silaha, na wengine walikuwa wanataja wahalifu ndani ya jamii na nilipata ushirikiano wa kutosha.''
Aidha Dkt. Mrema amesema anachokitafuta Rais Dkt. John Magufuli ni mtu mzalendo na hatua ya Rais kumteua ni kuonesha imani yake kwake na si kwamba ana nia ya kuua upinzani bali ana lengo jema la kuchukua mtu mwenye uzoefu ili atumikie watanzania kwa sababu lengo la upinzani siyo kutaka wananchi wateseke.
''Watanzania wategemee ufanisi na kazi iliyotukuka ya kupunguza wafungwa magerezani ili waweze kupewa adhabu nyingine ndani ya jamii na wapewe watu wa kuwasimamia, kwa kuwa tatizo kubwa tulilonalo sasa hivi ni mlundikano wa wafungwa na serikali haiwezi kujitika kutanua magereza kwa kuwa sasa hivi inajikita kuboresha huduma za afya na elimu mfano suala la madawati'' Amesema Dkt. Mrema
Kuhusu yeye kuwa mzee na kama ataweza kumudu nafasi hiyo Dkt. Mrema amesema yeye ana miaka 72 na hana uzee wowote ambao utamfanya akwame kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na hata kabla ya uteuzi Rais ana watu wa kumshauri na wameona anafaa nafasi hiyo
Rais Magufuli Anaishi Kwenye Maneno Yake Hana Longo Longo - Mrema Afunguka
5
July 17, 2016
Tags
Asante sana Rais Magufuli kwa kumchagua mchapakazi na mzalendo mweshimiwa Mrema. Mungu akubariki sana. Mimi ninao ushauri wangu kama mtakubaliana na mimi. Kwanza kwanini kuna mirundikano mingi ya wafungwa. Sababu ni kwamba wafungwa wengi walioko magerezani wengi wameonewa!! Wamebambikizwa kesi ambazo sio za kwao!! ( Ili ni kosa sana la kumsingizia binadamu mwenzako na kumfunga kwa kosa ambalo hajalifanya. Wafungwa wengi wanafungwa kwa makosa madogo madogo ambayo wangelifanya adhabu nyingine badala ya kutumikia vifungo mfano: Kwanini unamfunga mzuluraji,kama ametokea kijijini kutafuta kazi, akikosa kazi arudishwe nyumbani kwao akabidhiwe kwa mwenyekiti wa kijiji, apatiwe kazi za kufanya akirudi mjini apewe adhabu nyingine. ( Ukiniuliza garama za kumsafirisha zitatoka wapi, je garama za kumlisha kwenye jera zinatoka wapi? Nina mengi ya kuandika ila nina amini mweshimiwa Mrema utafanya kazi yako kwa uwaminifu wa kweili. Mwisho nakupongeza sana Rais wetu wewe ni kiongozi ambaye una muheshimu na kumuogopa Mungu. Mungu akurinde wewe na familia yako na watanzania wote.
ReplyDeleteJames Kalugira USA.
mrema una ukimwi au nini sababu unaonekana kama una ukimwi pia unaonekena choka ile mbaya
ReplyDeleteHata kama unamchukia hukupashwa kumsema hivyo,kumbuka wewe ni binadamu hujafa hujaumbika.
DeleteWEWE KICHAA,HATA KAMA MREMA ANGEKUWA NA UKIMWI,HIVI HICHO KICHAAA CHAKO NA MGONJWA WA UKIMWI BORA YUPI?
DeleteKuna watu yaani bado ni washenzi washamba vichwani mwao hasa huyo hapo juu aliyeandika kuwa Mrema sijui ana ukimwi kama ulikuwa huna cha maana cha kutoa mawazo yako si ungemezea tu au ili mradi uandike upuuzi wako tu wakati huyo mzee alipokuwa waziri wa mambo ya ndani nafikiri ulikuwa haujazaliwa bado mama yako alikuwa bado kigoli jaribu kufuatilia back ground ya Mrema utaona alikuwa ana nia gani na wananchi wa Tanzania kudadeki umeniudhi sana baradhuli wewe
ReplyDelete