Juzi Chama cha Demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’ kilitangaza mikakati mitatu ya kupinga ilichokiita ukandamizaji wa haki na demokrasia na kuitangaza siku ya September mosi mwaka kuwa ni siku ya maandamano nchi nzima.
Jana July 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo alizungumza na wananchi wa Manyoni Singida na kutoa onyo kwa watakaoanzisha maandamano.
"Wasije wakanijaribu mimi ni tofauti sana, na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa, siasa nzuri wananchi wetu washibe, wapate madawa, nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni"- Alisema Rais Magufuli
Hapa chini ni sauti ya Rais Magufuli sehemu ya kwanza na ya pili. Msikilize.
Sehemu ya Kwanza:
Sehemu ya Pili:
Rais Magufuli: Chadema Msiwape Vijana Viroba Ili Watangulie Kwenye Maandamanmo....Tangulieni Ninyi Viongozi Wao Ili Mkione Cha Mtema Kuni
11
July 30, 2016
Tags
Mimi kama mpinzani sitofanya hayo maandamano, watangulie kwanza viongozi wangu, mimi nitasubiri siku ya kampeni2020.huu naona kama uchochezi, nchi yetu ni ya amani, itabaki kuwa ya amani, mi mambo ya siasa uchwala nawaachia viongozi wangu Chadema
ReplyDeleteSijawahi kudikia rsidi yryote wa nchi snayepanga namna gani vyama vifanye mikutano yao .kuwaamulia viongozi wote wa nchi kama hawana elimu, hawana akili ni kosa. Raisi kazi yake di kutoa amri kama anarndesha jeshi.Raisi kazi yake inambidi ajue namna gsni ashirikiane na viongozi wote na wananchi ili kazi yake irahisishiwe kusudi makududio, malengo na mipango ya kazi zake zirahisishiwe. Mtu mmoja kwa amri hii nchi haitafika mbali, haitakuwa na amani nakumbuka enzi za Banda Malawi. Uhuru wa watu, namna ya kuongea na watu na kuwahedhimu watu itamrahisisia kazi kama raisi wa nchi. Hivi ni vitisho.unapowatisha, kueadharau. Na kulazimisha sheria zisizokitabuni, ni chsnxo cha machafuko. Hakuna kiongozi yeyote ambaye yupo juu ya sheria za nchi. Na sheria za nchi inabidi zimlinde kila zmtsnzania sawa. Hii ni hstsri kubes inayojionyesha wazi nchini. Ni hatari. Nadhani anawashauri wazuri. Kama hana eeee.inashtua.
ReplyDeleteWeee hizo nchi zetu za Africa ni corrupition tupu mtu aweza pewa. Kazi ya juu hata Elimu hanaa, maana yake nini. Elimu inatakiwa sanaa hasa katika nyakati hizo za utandandawazi hatutaki viongozi au wafanyakazi mangungo
DeleteKati ys sifa za uongozi ni amani ya moyo , utulivu usikivu ,kutafakari mambo kabla ya kusema, hekma. Ibads ili mungu skuingie ili uwe na utashi safi utuyumie kabla ya kusema kuzungumza na kutenda. Ama itskuwa ni maxoea kufanya makosa yale yale mara nyingi ksma tulivyoshuhudia tengua tengua nyingi zilizoyokea. Then hutakuwa serious na kazi kubwa uliyokabithiwa.ushauri. kuupokea bila kuuons ni challenge. Asiyekubali kuchallenjiwa ni rshisi sana kujihami na kuwachsllenge wengine. Pre emptive.na ile ni hatari. Unaweza piga bomu na kuua kwa hisia.
ReplyDeleteMzee Makamba alishawaambia, kama JK aliwabatiza kwa MAJI, JPM atawabatiza kwa MOTO.......nadhani tarehe 1/9/2016 ndio siku yenu rasmi ya kubatizwa kwa MOTO......mjiandae kwa 'sherehe'
ReplyDeleteNdugu inaonekana unapitwa na mengi......!!!, Mzee Makamba alimaanisha kama JK aliwabatiza wanaCCM kwa MAJI(aliwaongoza kwa kufuata sheria,utu na katiba ya chama) basi JP atawabatiza kwa MOTO((atawaongoza kwa AMRI,VITISHO pasipo kufuata sheria,utu na katiba ya chama). Uwe makini na kauli za Mzee Makamba maana wengi sana wanashindwa kutohoa sentensi zake.
DeleteHapo kusema viloba si haki kwa maana vijana nao wana utashi! sasa watapewa viloba maelfu ya watu itawezekana kweli!! wajue wao ccm wamewakosea watz wengi kwa kusitisha bunge live, viongozi wao waliowapenda kunyimwa nafasi ya kuzungumza nao n.k. n.k. wangekaa chini warekebishe baadhi ya mambo waone kama mambo hayatakuwa mazuri nchini... Mbona wakati wa JK wapinzani walimwandalia hadi chai! ni kwasababu alikuwa anameet their heart. Period Ubabe ni janga la kitaifa....
ReplyDeleteKuna Tatizo Namna Mtukufu Rais Wetu Mpendwa Anavyoamini Juu ya Uwepo wa Vyama vya Upinzani na Inaonekana Hataki KUAMINI Faida Zitokanazo na Uwepo wa Upinzani Tanzania Hasa Katika Kufichua Makosa Na Kurekebisha Makosa ya Kiutendaji Yanayosababishwa na Serikali.Namshauri Mtukufu Rais Wetu Aongoze Nchi Akijua Yeye Ni Baba na Si Tu Ana Jukumu la Kusimamia Wadogo Zetu Bali Pia Afahamu Anao Watoto Ambao ni Watu Wazima Wenye Utashi Uliotosheleza Kuwa na Uwezo wa Kuongoza Familia Hii.Kwa nchi yetu Tanzania Hatuhitaji Rais MKALI mwenye kuamini katika AMRI bali Tunahitaji Rais MKALI mwenye kuamini katika SHERIA NA BUSARA.
ReplyDeletedikteta uchwara
ReplyDeleteMagu hii ni Tanzania umeikuta na utaiwacha
ReplyDeleteUsitishe watu kiasi unapoteza imani kwa watanzania
Wewe ni rais wa wote usilazimeshe watu wote wakupende
Mmmhhh nyie ndio corrupti msiopenda maendeleo ya bara hili la Africa, hebu jaribu kitokacho basi muone na kwa wenzenu kwanza, maanake mmegubikwa na ujinga ulioptopea
Delete