Sare ya TP Mazembe v Mo Bejaia yazidi kuishindilia Yanga mkiani

TP Mazembe imejiongezea pointi moja baada ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya wenyeji wake Mo Bejaia katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

TP Mazembe walikuwa wageni wa Bejaia katika mechi ngumu usiku wa kuamkia leo na watakuwa na furaha baada ya kupata pointi hiyo moja muhimu.

Sare hiyo imeihakikishia TP Mazembe kufuzu hatua ya nusu fainali kwa asilimia 90 kwa kuwa kama itashinda mechi moja katika mechi tatu zilizobaki basi itakuwa ina uhakika wa asilimia 100.

Lakini sare hiyo, imezidi kudidimiza matumaini ya Yanga kuamka angalau na kupata pointi zitakazoiwezesha kubadili mambo kwa kuwa ina pointi moja tu baada ya kucheza mechi tatu ikipoteza mbili na kupata sare moja tu dhidi ya Medeama.


TP Mazembe inaendelea kuongoza kundi hilo ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Bejaia yenye tano, Medeama ina mbili na Yanga inaburuza mkia na pointi hiyo moja.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahaha!Wakimataifa wanasema bado wana nafasi ya kufanya vyema.
    Ila tukiacha ushabiki pembeni,Simba tunatakiwa tujipange kwa Yanga hii ninayoiona kila siku kwa sasa.Nimeona mazoezi ya simba morogoro kiukweli bado simba haileti matumaini ikikutana/itakapokutana na Yanga,kama hawatakaza tutegemee aibu nyingine kutoka kwa yanga japo mpira hautabiliki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. BORA UMESEMA UKWELI,NA MSITARAJIE UBINGWA ACHA TU YANGA IWE NI YA KUSHIRIKI KILA MWAKA LAKINI SIO SIMBA.NADHANI MWAKANI MTATUMIWA NDEGE NA WAARABU KWENDA KUWASHANGILIA.

      Delete
    2. MAVUGOOOOO

      Delete
    3. Mavugo wapi,kasema anatamani kucheza huko mbelembele huko lakini sio TZ na labda ingekuwa AZAM,au YANGA,Kwa hiyo msubiri akikosa timu huko mbele ndio atakuja labda.Na hapo ndipo muamini watu wanataka uki-mataifa.

      Delete
  2. Hongera Tp mazembe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad