Baada ya Bei ya POGBA Kuwa Gumzo Duniani, Scholes Ametoa Kauli yake

Paul Scholes anaamini kwamba Manchester United hawatakuwa wanatenda haki endapo watatoa kiasi cha paundi mil 92 (euro mil 110) kuinasa saini ya Paul Pogba kutoka Juventus, ada ambayo inaelezwa kuvunja rekodi ya usajili duniani.

Scholes ni shabiki mkubwa wa Pogba lakini amesema kwa bei hiyo inaaminisha kwamba uwezo wake ni sawa na Lionel Messi and Cristiano Ronaldo huku akisema haamini kwamba Mfaransa huyo ana thamani sawa na wakali hao wawili.

“Alikuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, Nimewahi kucheza naye mara nyingi tu,” Scholes aliwaambia wanahabari.

“Ni kweli amekuwa kwenye kiwango bora lakini bado siamini kama ana thamani ya paundi milioni 100 kwa sasa.”

“Kwa bei kama hiyo, ungehitaji mchezaji ambaye anaweza kufunga magoli zaidi ya 50 kwa msimu, kama Ronaldo au Messi, Pogba bado hajafika huko kabisa.”

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sio kumkandamiz ila kaongea ukweli. Pahal pa kutoa hiz pesa kwa Pogba afadhali nizitoe kwa Neymar kwan anauwez wa kufung, kund nafas nzur zakufung na anauwez wa kujitengenezea mwenyew nafas ya kufung kulik Pogba. Belle hakuwa na uwez wa kununuliwa zil pesa zote ila Ulaya inapend ishikilie rikodi zote ili pasiw mchezaj wa kutok Amerika kusin atakae chukua rekodi. Mfano Messi ana balld'or ngapi? kwa sasa wanafany kilakit iwezekanal Ronaldo nae ashinde ili wawe sawa kama walivy fany wakat wanamnyima Tiery H wakampaa Zinedine Z ili alingan na Ronaldo9. So ukitazam vizur utaon ukweli hapo.

    ReplyDelete
  2. Acheni ujinga huo huyu mweusi huyu mweupe wote ni viumbe vyake Allah swt, mbona nna fikra finyu lini mtaacha kasumba hizi hapo jamaa anataja kiwango cha messi na Ronaldo na wala sio rangi acheni kasumba hizo badilikeni kwani dunia haichukui mambo kama hayo mfano jamaa yule katika kuadhimisha sherehe Zanzibar anasema bila aibu kuwa hii nchi si ya machotara sasa nini maana yake maneno Kama Yale Kama si ubaguzi wote ni viumbe vya Allah swt na usimbague mtu kwa Dini Au rangi utakuja juta baadae

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad