Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda hajakubaliana na kitendo cha Rais John Magufuli kutoa fedha taslimu kwa ajili ya kuchangia safari za Hija akisema angezungumza na wahusika ili kujua matatizo ambayo fedha hizo zingesaidia.
Hata hivyo, amempongeza Rais kuahidi kurejesha mali za Waislamu.
Sheikh Ponda, ambaye alipiga simu ofisi za Mwananchi jana asubuhi, amesema ahadi hiyo ya Rais ni ya kuungwa mkono kwa kuwa inaonyesha kujali masilahi ya wananchi, hususan Waislamu.
Juzi, akihutubia Baraza la Idd el Fitr jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema atawasaidia Waislamu kurejesha mali zao na kumpongeza Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakar Zubeir kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kurejesha mali hizo kabla hata hajapewa cheo hicho.
Unapotoa mchango kwa jamii kwa hiari yako hupashwi kuuliza unayemtolea anashida au mapungufu kiasi gani,ukumbuke hapo waislam hajaomba chochote kwa ajili ya hija kutoka kwa rais bali ni rais mwenyewe ameona awachangie alicho nacho.Nimependa pia hajasema ni kiasi gani na hiyo ndio maana ya sadaka.
ReplyDeleteHv kutoa fedha taslim si ndo kusaidia matatizo yaliyokuwepo au...huyu babu alitalaje mkuu wa nchi keshajipatoa thawabu yake hapo kwa kufadhili hiyo hija sooo stop complaining...just sit back n relax mnachefua sometimes sio kila kitu lazma uongee
ReplyDeleteHahahahahahaha,hajasikika siku nyingi,na hapo yeye Ponda ndio alipiga simu mwananchi yote kutaka aandikwe tu.
DeleteNikukosoe/nikuulize sheih Ponda,kwani ukipewa hela ununue gari na wakati huna nyumba huwezi kubadilisha kwa kununua nyumba/kiwanja kwa kuona kiwanja ni bora kwako kuliko gari?
ReplyDeleteRais ametoa mchango kwa ajili ya hija
lakini kama wahususika wataona maandalizi ya
hija yamekamilika kwani kuna kikwazo pesa hiyo
kuingia kwenye hitaji lingine?
Huyu babu nae sijui anaongea nini mweeh.
ReplyDeletenyie hamumjui mtumbua majipu...analopanga yeye kamwe habadilishegi la sivyo atamtumbua mtu jipu....ndo maana sheikh ameomba au amependekeza iwe hivyo..nitahazari kabla ya hatari...anamaana yake kusema hivyo sio bure... hajakosea-.
ReplyDelete