Sheikh Ponda Issa Ponda Amshukia Magufuli

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini (JTK), Sheikh Ponda Issa Ponda amesema, ni mapema mno kufurahia kauli ya Rais John Magufuli kuwa atarejesha mali za Waislam zilizoporwa na wajanja wachake. anaandika Mwandishi Wetu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Sheikh Ponda amesema, “tunasubiri kuona utekelezaji wa kauli hiyo. Kama ni kweli imetoka moyoni, tutaiona.”

Hata hivyo, Sheikh Ponda amesema, “ipo mikataba mingi ya kifisadi iliyogharimu mali za Waislam. Nashukuru rais kutambua hilo na ikiwa atalitekeleza kwa vitendo, basi litakuwa jambo jema.”
Akizungumza katika Baraza la Eid lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alidai kuwa serikali yake itarejesha mikononi mwa waumini wa kiislamu mali zao zilizoporwa.
Alisema, kumekuwepo na malalamiko kwa taasisi hiyo kudhulumiwa mali zake na wafanyabaishara wajanja.

Alisema, “nakumbuka nilipokuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, viongozi wa Bakwata mlikuwa mnakuja ofisini kwangu kulalamika juu ya suala hili. Leo nimekuwa rais, nitazirejesha.”

Amesema, “niliwaambia wakati ule kwamba wanawadaganya, mnaingia nao ubia kumbe ni matapeli.”

Kutokana na dhamira hiyo, Sheikh Ponda amesema kuwa, yeye pamoja na Waislam wote wanapongeza hatua hiyo na wanasubiri kuona utekelezwaji wake.

“Mimi binafsi napongeza hatua hiyo, hatua ya kupitia mikataba ya kifisadi ni jambo jema. Kwa upande wetu, tupo tayari kutoa ushirikiano wowote unaohitajika.
“Tupo tayari kusaidia kutoa nyaraka zinazobeba ukweli juu ya jambo lililofanyika. Lengo letu ni kuona kile ambacho kimeporwa kinarejeshwa kwa wahusika.”
Akizungumzia hatua ya Rais Magufuli kutoa “ruzuku” kwa ajili ya kusaidia kusafirisha Waislam wanaokwenda kutekeleza ibada ya Hijja ambayo ni Nguzo ya Tano katika dini ya Kiislamu, Sheikh Ponda amesema, “ni fikra nzuri kusaidia katika Hijja.

Hata hivyo, Sheikh huyo machachari nchini anasema, “lakini naamini uhitajio mkubwa katika taasisi za dini ni kuboreshwa elimu na afya, siyo Hija.”

Anaongeza, “ingekuwa vizuri zaidi kama fedha hizo rais angezielekeza katika masuala ya kuboresha elimu na afya kwenye taasisi za Kiislam.”

Chanzo:Mwanahalisi
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Udaku na Mwandishi aliyea andika... Maudhui ni nzuri na inastahili kupewa pongezi. Ina nia njema na Kuthibitisha kuwa Waislamu wameipokea Vizuri na Wanasubiri kwa hamu utekelezaki wake...

    Kibaya katika hii ni KICHWA CHA HABAR HAKISTAHILI WALA HAKIENDANI na MAUDHUI ya NIA NJEMA aliyo Onesha Raisi Wetu JPJM.. Neno Amshukia limeshindwa kuleta Uelewa ma mantiki Halisi ya Nia Njema na inaleta Upotofu ikiwa utasoma kichwa cha habari.. Ndugu zangu sisi hatujengi Chuki tunajenga Umoja / Mshikamano na Upendo ili tupate kujuana na kusaidiana...

    Naomba Muandishi wa kichwa cha Habari na Mhariri wawe wanarudia Vichwa kabla ya Kuruhusu kuingia katika Mitandao yetu .. Ili tuweze kuambatanisha Maudhui na Uwiano na Kichwa Husika. EID MUBARAK

    ReplyDelete
  2. Udaku na Mwandishi aliyea andika... Maudhui ni nzuri na inastahili kupewa pongezi. Ina nia njema na Kuthibitisha kuwa Waislamu wameipokea Vizuri na Wanasubiri kwa hamu utekelezaki wake...

    Kibaya katika hii ni KICHWA CHA HABAR HAKISTAHILI WALA HAKIENDANI na MAUDHUI ya NIA NJEMA aliyo Onesha Raisi Wetu JPJM.. Neno Amshukia limeshindwa kuleta Uelewa ma mantiki Halisi ya Nia Njema na inaleta Upotofu ikiwa utasoma kichwa cha habari.. Ndugu zangu sisi hatujengi Chuki tunajenga Umoja / Mshikamano na Upendo ili tupate kujuana na kusaidiana...

    Naomba Muandishi wa kichwa cha Habari na Mhariri wawe wanarudia Vichwa kabla ya Kuruhusu kuingia katika Mitandao yetu .. Ili tuweze kuambatanisha Maudhui na Uwiano na Kichwa Husika. EID MUBARAK

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swadakta Sheikh hapo juu umenena haswa kuhusu hicho kichwa cha habari cha hapo juu kwenye "Amshukia"wallahrahadhim kiswahili ni kigumu sana haswa kwa watu waliotokea mbali na sehemu za mwambao Sheikh kinawapa tabu sana hiki kiswahili maana jinsi wakizungumzavyo na wakiandikavyo ni vitu viwili tofauti visivyoshabiiana kabisa kwa jumla hawakielewi japo wengi hutokwa na mapovu kuwa ni lugha yetu ya taifa sasa kama ni lugha yako ya taifa iweje hauielewi?

      Delete
  3. Sasa hapo kamshukiaje?

    ReplyDelete
  4. UANDISHI WA KICHOCHEZI,KAMSHUKIAJE?MBONA KICHWA CHA HABARI NI CHA KISHARI WAKATI STORY NI YA AMANI?

    ReplyDelete
  5. NI KWELI KICHA CHA HABARI HAKIENDANI NA STORY YENYEWE!!!

    ReplyDelete
  6. Huyo sheikh naeeee kila kitu lazma upinge khaaa mnaboa sasa...juhudi zikionekana pongezaaa sio kila kitu lakn laknn..khaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana Mdau, kama utakumbuka hata Mh. Kassim Majaliwa alizungumzia uimarishaji na utumiaji wa Lugha yetu ambayo ukiangalia chimbuko lake zuri lipo kweetu sisi WATANZANIA.. nA ZAMA ZILE Kama utakumbuka tulikuwa na vipindi maalum vya MBINU ZA KISWAHILI na Matumizi ya Lugha na tukawa na Baraza la lugha.. na vitabu vingi vizuri na washairi wngi wazuri kama kina marehemu SHAABAN ROBERT NA WENGINE WENGI.. HII ILIWEZA KUBORESHA LUGHA NA MATUMIZI YAKE.. LEO TUSINGE PATA TABU SANA KUONA WAHESHIMIWA WETU WANALETA LUGHA ZISIZO KUWA NA MAADILI NA VIJANA WETU KUKOSA MENGI KATIKA UELEWA WA LUGHA ... SASA NI BORA SISI WATANZANIA TUIBORESHE NA KUITUMIA IPASAVYO NA KUREKEBISHA MISAMIATI YETU ILI VIJANA WETU WA KARNE HIZI ZA TECHNOLOJIA WAWEZE KUPATA NA KUITUMIA LUGHA SAHIHI NA IPASAVYO .. NA NI IMANI YANGU TUKIWEZA HILI UPOTOSHAJI UTAKUWA MCHACHE KAMA SI KUKOSEKANA KABISA.
      NADHANI UTAKUBALIANA NAMI... SABABU NI SISI MIMI NA WEWE TUNAHITAJI KUIPELETA HII LUGHA DUNIANI NA UKWELI INATUMIKA NCHI NYINGI. NA KUNA WATU NIMEWEZA KUWAKUTA WANAZUNGUMZA NCHI AMBAYO SI LUGHA YAO NIKAWAULIZA HII LUGHA YA WAPI.. HAWAJUI ILA WANASEMA TOKA BABU ZAO WANAZUNGUMZA NA JAMII YAO WANAJUANA KWA LUGHA HII(KISWAHILI) NA HAWAJAPATA HATA KUFIKA HUKU KWETU..NAOMBA TUIJUE NA TUITUMIE IPASAVYO NA IWE MAHALI PAKE.. NAJUA MAZOEA TUNAWEZA KUYASAHIHISHA.. ASANTE KWA UEKEWA WAKO..

      Delete
    2. Hapana Mdau, kama utakumbuka hata Mh. Kassim Majaliwa alizungumzia uimarishaji na utumiaji wa Lugha yetu ambayo ukiangalia chimbuko lake zuri lipo kweetu sisi WATANZANIA.. nA ZAMA ZILE Kama utakumbuka tulikuwa na vipindi maalum vya MBINU ZA KISWAHILI na Matumizi ya Lugha na tukawa na Baraza la lugha.. na vitabu vingi vizuri na washairi wngi wazuri kama kina marehemu SHAABAN ROBERT NA WENGINE WENGI.. HII ILIWEZA KUBORESHA LUGHA NA MATUMIZI YAKE.. LEO TUSINGE PATA TABU SANA KUONA WAHESHIMIWA WETU WANALETA LUGHA ZISIZO KUWA NA MAADILI NA VIJANA WETU KUKOSA MENGI KATIKA UELEWA WA LUGHA ... SASA NI BORA SISI WATANZANIA TUIBORESHE NA KUITUMIA IPASAVYO NA KUREKEBISHA MISAMIATI YETU ILI VIJANA WETU WA KARNE HIZI ZA TECHNOLOJIA WAWEZE KUPATA NA KUITUMIA LUGHA SAHIHI NA IPASAVYO .. NA NI IMANI YANGU TUKIWEZA HILI UPOTOSHAJI UTAKUWA MCHACHE KAMA SI KUKOSEKANA KABISA.
      NADHANI UTAKUBALIANA NAMI... SABABU NI SISI MIMI NA WEWE TUNAHITAJI KUIPELETA HII LUGHA DUNIANI NA UKWELI INATUMIKA NCHI NYINGI. NA KUNA WATU NIMEWEZA KUWAKUTA WANAZUNGUMZA NCHI AMBAYO SI LUGHA YAO NIKAWAULIZA HII LUGHA YA WAPI.. HAWAJUI ILA WANASEMA TOKA BABU ZAO WANAZUNGUMZA NA JAMII YAO WANAJUANA KWA LUGHA HII(KISWAHILI) NA HAWAJAPATA HATA KUFIKA HUKU KWETU..NAOMBA TUIJUE NA TUITUMIE IPASAVYO NA IWE MAHALI PAKE.. NAJUA MAZOEA TUNAWEZA KUYASAHIHISHA.. ASANTE KWA UEKEWA WAKO..

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad