Shela ya Harusi Aliyovaa Nancy Summary Siku ya Harusi Yake Yazua Gumzo


Shela alilovaa Miss Tanzania 2005, Nancy Abraham Sumary alipokuwa akifunga ndoa na mchumba’ke, Lucas Neghesti mwishoni mwa wiki iliyopita, limezua gumzo kutokana na ‘usimpo’ wake licha ya gharama yaku kuwa kubwa ambapo linadaiwa kununuliwa kwa shilingi milioni tano za Kitanzania.

 Kwa mujibu wa chanzo chetu, kisa cha kuzua gumzo ni jinsi lilivyokuwa simpo kwa muonekano ingawa lilimpendeza na kumtoa chicha kwani wapo waliopenda namna lililofanana na lile la mdogo wake staa wa muziki Marekani, Beyonge Knowles, Solange Knowles ambalo ndiyo lilitakiwa kuwa na gharama kubwa kwani linastahili kutokana na kuwa limeshavaliwa na staa huyo wa Marekani.

Hata hivyo, wapo waliomsifia kwa jinsi alivyojidizaini na kuwa bibiharusi simpo na mwenye muonekano wa kimataifa kwani kwa Watanzania wengi imekuwa ni vigumu mwanamke kufunga ndoa akiwa na nywele zake (natural) tofauti na wengine ambao hupenda matashtiti kibao.

Nancy na Luca walifunga ndoa Ijumaa iliyopita ambapo mrembo huyo alivaa kikofia kilichodizainiwa na mwanamitindo mfaransa na fasheni yake ni ya mwaka 2016 huku mumewe akivalishwa na mwanamitindo, Martin Kadinda
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wabongo bana mtu kwenye harusi yake anaweza kuvaa jinsi anavyotaka mwenywewe bila kumjaji, kama mdogo Wake na beyonce alipofunga harusi mbona yeye na mume Wake waliendesha baiskeli kurudi nyumbani ingawa wanayo magari ya kifahari

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad