Shibuda: Msindai, Mpendazowe Wanafiki

HATUA ya Fredy Mpendazowe na Mgana Msindai kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatokana na kuhangaikia maslahi binafsi, anaandika Dany Tibason.

Msindai, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa madai, ndani ya CCM hakuna demokrasia.

John Shibuda, Katibu Mkuu wa Chama cha ADA TADEA amesema, wakongwe hao katika siasa waliondoka CCM kwa madai ya kukerwa na chama hicho lakini cha kushangaza wamerejea kwa mbwembwe.

Shibuda amesema kwamba, wanasiasa hao ni wanafiki ndani ya siasa na kuwa “mnafiki hafi hadi ameumbuka.” Amedai hatua ya kurejea CCM imewaumbua.
“Waliishambulia CCM wakiwa kwenye majukwaa ya Chadema, leo wamerejea kule walikokuwa wakishambulia,” amesema Shibuda.

Amesema, Mpendazowe na Msindai wamekuwa wakiuaminisha umma kwamba CCM ni chama cha hovyo “iweje leo warejee kule kule kwa hovyo?

“Watu wazima kama hao ni wanafiki ndani ya siasa na wamekula matapishi yao. Hawawezi kuaminika tena katika jamii na katika ulingo wa siasa kwa kuwa, ni wanasiasa maslahi.
“Siyo wanasiasa bali wamevaa vazi la siasa huku uhalisia ukiwa ni wanasiasa maslahi. Hakukuwa na maana kutumia majukwaa kuitukana CCM na baadaye kurudi.

“Walipotoka CCM kwenda Chadema walitumia majukwaa kuishambulia CCM na sasa wamerudi CCM kwa kuishambulia Chadema.”

Shibuda amesema, umri wa wanasiasa hao ulitakiwa kutumiwa kuwajenga vijana kifikra juu ya kuwepo kwa siasa safi ambazo ni za ukombozi.

“Kwa umri wa Msindai na Mpendazowe walitakiwa kuwa shamba darasa na urithi wa mawazo kwa vijana chipukizi wa kisiasa.

“Tujikumbushe jinsi Mpendazoe alivyoweza kutunga kitabu ambacho kiliweza kuelezea mambo mengi, leo ni aibu kwa msomi huyo kuonesha udhaifu wa kisiasa na kujidhalilisha,” amesema Shibuda.

Pia ameishangaa CCM kwa kuwapokea wanasiasa wachafu na ambao wamekuwa wakikisema chama hicho vibaya hadharani.

“Kauli ya Rais John Magufuli kudai anataka usafi ndani ya chama ni unafiki, sidahi kama kuna kanisa ambalo linaweza kumpokea muumini ambaye aliyemkataa Yesu au msikiti ambao unaweza kumkaribisha muumini ambaye alimkataa Mtume.

“Je, muumini wa Dini ya Kiislamu anaweza kuitukana Qur’an na baadaye akaanza kuisifia? hilo jambo haliwezekani.”
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Heeh! Hivi huyu jamaa nayeye yupo!! Wewe Shibuda ndio manafiki, ulitoka CCM, ukahamia Chadema, nako umetoka uko wapi sijui kutafuta vyeo......na bado utazunguka sana.....wengine wanatamani kurudi ila wanaona aibu, hata wewe usione haya, rudi tu CCM. Eti unashangaa hao watu kupokelewa tena CCM, tena bila aibu unatoa mifano ya kanisa na msikiti, kwani hujui vitabu vya dini vinasema samehe 7x70?? Au nawewe huna dini kama Kingunge?? UMEISHIWA.

    ReplyDelete
  2. Watanzania fungueni macho
    WANAFIKI HAPA ni CCM
    Watu hawa walihama ccm kwa vishindo na kukashifu CCM
    Leo wanerudi CCM
    Tena wanapokekewa kwenye kikao cha juu cha CCM
    Hijatokea duniani kote
    Rais na mwenyekiti kupokea wasaliti hawa !
    CCM mnatisha na ni aibu aibu aibu aibu aibu
    Yote haya ni Lowassa tu!!!!!!!?!!??
    Au kingine !!!!????

    ReplyDelete
  3. Hahaaaa shibuda wanasiasa ndivyo mlivyoo hata mbowe alituaminisha lowassa f isadi mbona alimpokea kwa mbwembwe nakupewa nafasi ya kugombea urais mmezoea kuchezea na akili za watu mxyuuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lowassa tofauti na hawa na hakupokelewa Kama hawa acha ushamba
      Lowassa alifanyiwa zengwe ccm
      Pia Sumaye

      Delete
    2. we anony 2.07am acha upumba wako Lowasa si ndiye alikuwa anatukanwa kila siku na Chadema kwamba ni fisadi papa??? Sumaye si ndiyo alikuwa anaitwa Mr Zero na hao Chadema???? zengwe gani alofanyiwa huyo Lowasa wakati tulishajua akiwa mgombea hata robo kura hatutapata kwa kuwa mlikuwa mnaujua ufisadi wake???? acha uzembe wa kufikiri, tumempata JPM mwacheni atunyooshe kwanza

      Delete
  4. Chadema hata zitto arudi atapokelewa na mwenyekiti wa mtaa
    Ataanzua hukoo

    ReplyDelete
  5. Poleni sana hii ndiyo BONGO karibu sana ila mifano yako ya ulinganishi wa dini au waku wa dini si mzuri ondoa jaziba siasa za Bongo siyo za kulinganishwa na dini wala waumini wa dini
    Hivi unajua mtu huwa amesoma masomo ya dini kiasi gani hadi kuitwa Askofu??? Bongo ukimaliza tu darasa la saba unaweza kuwa ASKOFU wa kanisa!!!! hahhhahhaa Waheshimu maaskofu wa TZ weeeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad