Shilole alalamika kufanyiwa udhalilishaji kwenye kivuko cha Kigamboni

Msanii wa Bongo Flava, Shilole amelalamika kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa amefanyiwa vitendo vya udhalilishaji katika kivuko cha Kigamboni, jijini Dar es Salaam.



Muimbaji huyo ameishia kulalamika tu na hakutaja hasa kitu gani amefanyiwa.

“Uzalendo maana yake nini??
Je kuna thamani yoyote kuwa mtanzania??
Je jitihada zozote zinazofanywa na wasanii kuitambulisha nchi yao zinathaminiwa??
Jana nimetendewa kitendo cha ajabu katika kivuko cha kigamboni na kutendewa udhalili bila kujali kuwa mimi ni mwanajamii nayegusa maisha ya watu.
Muziki ni biashara, lakini pia tuna nafasi yetu katika kuisaidia jamii na kupeleka ujumbe muhimu.
Tusiheshimiwe tunapohitajika na kudharaulika tunapohitaji tuheshimiwe.
Nimeguswa…. Nimeumia.
Someone should act. @paulmakonda @paulmakonda”

ameandika Msanii huyo

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama ulikuwa unajishaua sanaaa na kujiona wewe ndio wewe ufwati sheria, razima, kila sehemu jamii uieshimu nayo itakueshimu, sio swala la msaani kila mtu ana mchango wake katika jamii, wewe muimbaji, mwenzio mkulima au mfanyakazi hospital,nurse, mwalimu hata mvuvi wote wanamichango yao katika jamiii, kimataifa na kitaifa, toeni huo ujinga wa msaani. Nchi za ulaya msaani sijui nini ni kawaida sana. Kwa hiyo usijikweze wewe tafuta hela yako au kipato chako na huo usanii wako sio kujikweza

    ReplyDelete
  2. Haimuhusu mtu yeyeto zaidi yako na mashabiki wako,sasa hapo Makonda unataka afanye nini wakati wewe mwenyewe picha zinaonyesha ulikuwa unatoa ushirikiano na mashabiki wako kwa asilimia 100?Wangapi wanafanya shoo hawaguswi au kuchezewa mwili kama wewe?JIHESHIMU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad