Mrembo aliyezaa na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amefunguka kuwa, kuingia doa kwa penzi lake na jamaa huyo hakujamkatisha tamaa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye ni staa.
![]() |
Siwema na Nay wa Mitego |
Siwema ameliambia Wikienda kuwa hawezi kuapa kwamba hatakaa atumbukie tena kwenye penzi la msanii kwa kuwa hakuna anayejua huko mbeleni ataangukia kwa nani.
“Siwezi kusema kuwa Nay amenikatisha tamaa au sitaingia tena kwenye penzi la staa kwa sababu naweza kuapa halafu ikawa sivyo,” alisema Siwema.
hivi kuna staa bongo? mastaa bongo hawana tofauti na watu wa kawaida staa ni mtu anayejulikana duniani kote
ReplyDelete