UVCCM Yawapa Onyo Kali Vijana wa CHADEMA Walioandaliwa Kuvuruga Mkutano wa CCM Dodoma

Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) umeingia katika mvutano mkubwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuhusu Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho tawala uliopangwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma.

UVCCM wameionya BAVICHA kuhusu mpango wao wa kutaka kukusanyika mjini Dodoma siku hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa unakiuka amri halali ya polisi ya kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya kisiasa nchini.

Onyo hiyo limetolewa na  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka ambaye aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa watawakabili kwa nguvu zote BAVICHA endapo wataamua kuendesha siasa zinazolenga kuvuruga amani na kuleta hofu katika jamii na kutishia maisha.

Alisema umoja huo hautaona shaka kutumia mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau miongo kadhaa iliyopita nchini Kenya.

“Hatutaona muhali kupita njia zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili kukihami chama, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi na heshima yetu,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM.

CCM inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum Julai 23 mwaka huu ambapo Rais John Magufuli atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Weweeeee Shaka , wacha hiyo , comparing Mau Mau youth with Wimps ??? come on , most of you have never heard a Gunshot ,let alone holding a Gun , mbinu gani utatumia ? Mau Mau walikuwa wakipigana misituni na vita vya kushitukizia , Dodoma kuna Msitu ? wacheni Tisha toto zenu

    Kitisho hutishwa mwana mchanga hajiamili
    ambae hajalingana , upambanuzi wa feli
    watisha watu vijana , walokomaa Rijali
    Mungu akupe Akili hilo usifanye tena !

    ReplyDelete
  2. Swali langu ni hili kwa polisi. Hili ni tangazo was I la kivita toka vijana wa CCM. Ms umau il ikuwa vita juu us msituni.bunfuki, visu. Mbona hsmjamsika. Katsngaza vita wazi hsfharani. Sngrkuwa Mbowe au zlisu. Mngemeita na kumeeka ndani.hizi dheria za kupendelea Ccm zinaonrkans wazi. Watu n.a. viongozi wanafikiri n.a. kuendesha nchi kichams (kiccm)
    Hoi ni hstsri n.a. inapasua nchi. No tano la kulichukulia izigo wa hali ys juu. Hawa vijana wa ccm wsmebwa n.a. uongozi wa juu, wanaojua wanakinga na hawatafanyiwa chochote. Hi maringo waliyonayo sababu serikali inawalea. Hawatskuws hodari kwsni kwo kila kitu nirahisi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau mimi nina wasiwasi na utanzania wako khaaa!! kiswahili gani hicho ulichokiandika hapo unasoma mtu mpaka unapata kizunguzungu kudadeki

      Delete
  3. jeshi letu na serikali ikiruhusu mkutano huu nahakika watatengeneza uhasama baina ya watz,na hatar itakuja tokea cku c nyingi huko 2endako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad