Vanessa na Jux waenda vekesheni Serengeti, walipofikia kila kichwa hulipa shilingi mil 3.2 kwa usiku

Vanessa Mdee na mpenzi wake Jux wameamua kwenda kupumzika kwa muda kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti. Wawili hao wamelazimika kusimamisha ratiba zao ndefu za muziki na biashara kujionea maajabu kwenye mbuga hiyo maarufu duniani iliyopo wilayani Serengeti, mkoani Mara.

Wamefikia kwenye moja ya hoteli za mbugani bora zaidi duniani, Singita Serengeti Grumeti. Hoteli hizo zinazomilikiwa na wawekezaji wa Afrika Kusini, ni miongoni mwa hoteli zinazotoza gharama kubwa zaidi kwenye mbuga za wanyama barani Afrika.

Wawili hao wamefikia kwenye hoteli ya Faru Faru Lodge ambayo ni miongoni wa himaya za Singita zilizo katikati kabisa mwa mbuga hiyo kiasi ambacho wakati mwingine wageni huwezi kuwaona wanyama wakiwa wamejipumzisha kwenye vyumba vyao.

Kwa mujibu wa gharama za mwaka 2016 za kulala Faru Faru Lodge, katika kipindi hiki kinachojulikana kwa lugha za mbugani kama ‘high season’ ambacho huanzia June 1 hadi Octoba 31, suite ya bei rahisi zaidi (double/twin) hutoza dola 1,500 (zaidi ya shilingi milioni 3.2) kwa mtu mzima, kwa usiki mmoja (per adult per night).

Hiyo ina maana kuwa Vanessa Mdee na Jux wanalipa shilingi milioni 6.4 kwa usiku mmoja kulala Faru Faru Lodge. Hata hivyo Jux alianza kwa kufikia Sasakwa Lodge ambayo ina gharama kubwa zaidi kuliko Faru Faru. Yenyewe bei ya chini kwa usiku mmoja kwenye high season ni dola 1995 ambazo ni takriban shilingi milioni 4.2 za Kitanzania.

Akipost picha ya Vanessa akiwa kwenye Jacuzzi, mbele kukiwa na glasi mbili za champagne, akifurahia mandhari ya mbuga hiyo, Jux ameandika: Day 1 at Sasakwa Lodge was nice but the queen arrived on day 2 so we had to upgrade for that better view Farufaru is almost as dreamy as her #Tanzania #Serengeti #Vacation.”

Naye Vee kwenye picha hiyo hiyo aliyoiweka Instagram, aliandika: Reboot in session #SheKing #OurSingita. Kwenye picha nyingine aliandika #Day 1 at Faru Faru. Much needed vacay. #Safari #Tanzania #Serengeti #Africa #UtaliiwaNdani #OurSingita.”

Tazama picha zaidi:

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mapenzi yenu ya kiutu uzima. I aplaud you. Sio Wema na Idris utoto tu kichefuchefu. Wema please stop acting like a child!!

    ReplyDelete
  2. Kweli lakini. Wema ana act kama litoto lidogo kumbe li dada lizima mweee.

    ReplyDelete
  3. WAWILI HAWA WANAJIELEWA NA WAKO FOCUSED NA MAISHA YAO. SIO KINA DASH DASH DASH AMBAO NI WENGI WASIOJIELEWA.......BIG UP #JUXVEE!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. WAWILI HAWA WANAJIELEWA NA WAKO FOCUSED NA MAISHA YAO. SIO KINA DASH DASH DASH AMBAO NI WENGI WASIOJIELEWA.......BIG UP #JUXVEE!!!!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad