Inadaiwa Lissu alitoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya Kisutu kwa kumuita Rais ‘dikteta uchwara’, mtuhumiwa amedhaminiwa na wadhamini wawili na kesi imeahirishwa mpaka August 02 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa. Nje ya mahakama ya Kisutu, Lissu ameyazungumza haya……….
’Mimi nilidhani kwamba baada ya kauli yangu wenye busara wangenyamaza kimya lakini inaelekea busara inaonekana ni bidhaa adimu wameyaleta mahakamani, mimi na jopo langu la mawakili tutapata fursa ya kumuita huyo niliyemuita dikteta ‘uchwara’ kuja mahakamani kuiambia mahakama kuwa yeye si dikteta uchwara‘
Mtazame Hapa:
Hapo sidhani kama ni siasa tu kutoka kwa Lissu,bali kuna neno "SIKUBALI,NA LIWALO NA LIWE" Kitu ambacho ni kibaya kwetu.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDeleteHuyu Tundu kama sio bange basi ana walakini anatuaibisha kama taifa kwa ukosefu wake wa akili upinzani hauendi hivyo mpaka kumdhalilisha mkuu wa nchi kama anamuonea donge Magu asijifanye anatuwakilisha watanzania wote hatukubaliani nae kama anatumwa kuwa kibaraka wawa saliti ni yeye
ReplyDeleteMnachosha nyie watu,basi tu!
ReplyDeleteWee Lisu,hivi unajua kama asilimia kubwa ya watanzania wako tayari kushindia uji,au kula mlo mmoja kwa siku ili mradi tu amani iwepo?
ReplyDeleteEti mna uchungu na watanzania,mbona hamuachi posho kwa ajili ya wananchi?mbona mlio wengi hapo mna mashamba ambayo hamuyaendelezi wakati wako watu wanatafuta sehemu za kujenga au kulima?Ni uroho wa madaraka ndio unawasumbua,hamna lolote lingine.
Tundu Lisu nafikiri licha ya kuukusudia kwa makusudi kabisa kupotosha umma kwa hoja yake feki ya udikteta vile vile kama kunauwezekano wa kwenda kupimwa akili yake ingekuwa jambo la busara sana inawezekana kabisa yakuwa Lisu ni mgonjwa wa akili.Yeye kama sheria za nchi anazielewa basi kukamatwa au kushitakiwa kwake kwa utonvu wa nidhamu muheshimiwa raisi hana kuhusika kabisa na jambo hilo. Nchi au Tanzania sio Maghufuli peke yake. Wewe kwa akili yako vurugu zitokee tuseme uwanja wa mpira hivyo vyombo vya dola visuburi amri ya Magufuli kuwashughukia hao wanaofanya vurugu? Sawa na kesi ya Tundu Lisu karopokwa maneno ya kipuuzi na vyombo vya usalama vimeona kuna haja ya kumdhibiti kwa kuepusha uvunjifu wa amani sasa Magufuli anahusika na nini na kukamatwa kwa Lisu kama si kutaka kujitafutia umaarufu kwa kutumia jina la raisi? Wenye nchi ni vyombo vya usalama wa nchi Maghufuli sidhani kama ana time ya Lisu kasema nini hasa ukitilia maanani jinsi gani mkuu huyo wa nchi alivyo very busy na masuala muhimu ya maendeleo ya nchi yetu. Viongozi wa upizani huko nyumbani lazima wawe makini huko nyumbani na kauli zao za hovyo. Mara kadhaa hapa Marekani vyombo vya usalama vimehusika na baadhi ya matukio yanayohusika upotevu wa maisha ya watu mpaka Obama mwenyewe anafika kulalamikia matukio hayo hii ni kuonyesha yakwamba vyombo vya usalama vina mamlaka yale binafsi katika kutekeleza majukumu yao ya kiusalama. Sasa kwenda kumkashifu raisi wa nchi kwa kosa lako binafsi na vyombo vya usalama ni upumbavu wa hali ya juu hasa kwa mtu anaejiita mbunge na mwanasheria. Utaona hapa jinsi gani wapinzani walivyochanganyikiwa na kasi ya Magufuli.
ReplyDeleteUmaaruu kumbe ndio tatizo sio shida za wananchi, hivi jaalia kama Tanzania Rais awe Mh. Tundu Lisu ingekuwaje. Tengeneza hiyo Taswira halafu tafakari
ReplyDelete