Vijana Chadema Walianzisha Tena Dodoma

Vijana wa Chadema wanatua tena Dodoma ambako CCM inaendelea na maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mkutano mkuu maalumu wa kumkabidhi Rais John Magufuli kiti cha uenyekiti.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amesema wanatarajia kutua mjini humo kufanya mkutano wa kamati ya utendaji Julai 20 na Mwenyekiti wa chama chao, Freeman Mbowe atahudhuria.

“Polisi imepiga marufuku mikutano ya hadhara, siyo ya ndani. Sidhani kama kikao hiki watakizuia kwa sababu ni cha ndani,” amesema Katambi.

Amesema kikao hicho, kitajadili na kutoa mwelekeo wa masuala mbalimbali ikiwamo mkakati wao mpya wa kutafuta haki na demokrasia aliyodai inaminywa.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtakuja Na vigezo Na ubunifu ambao Nia Na Dhamira zenu zinaeleweka Na sisi yunazielewa..Ila kwa taarifa yenu Na hiyo nggoma yenu ya lele mama. Mtaicheza wenyewe sisi mi watazamaji Na mwisho wake unajulikana....Kuweni kiakili

    ReplyDelete
  2. Kutafuta hali Na Demoklasia?? Wapi huku? Haki Ni nini? Na Demokrasia nini?? Je Tuko katila uanaharakati?? Je sisi mi wazina au ... Mbona hatujielewi??

    ReplyDelete
  3. Mbona Edo aalizumgumza ya maana kiasi.. Uana harakati umeshapitwa ..sasa Ni lazima tukomae kisasa..mbo a mnatirudisha nyuma!! Msituharibie Chama chetu.

    ReplyDelete
  4. Katambi..Ajira ziko namna nyingi.. Na upoyezaji wakati pia iko Na njia zaidi ya moja. Je wewe unachokifanya Ni kipi?

    ReplyDelete
  5. Kama sio shari na lawama

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad