Vijana wa Chadema watii agizo la Mbowe..Viongozi Wao Kufikishwa Mahakamani Leo


Jeshi la Polisi limekwama kuwafikisha mahakamani viongozi wanne wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), baada ya kukosea hati ya mashtaka.

Wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Kasambala na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, George Tito.

Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema makosa yametokea wakati wa uandaaji wa hati ya mashtaka.

 “Mahojiano yameisha, charge sheet (hati ya mashtaka) ikaandaliwa, lakini ikarudishwa tuifanyie marekebisho. Muda umepita wa Mahakama watapelekwa kesho (leo),” alisema.

Hata hivyo, alisema kesi hiyo haina dhamana kwa upande wa kituo cha polisi na hivyo kuwalazimu watuhumiwa hao kuendelea kukaa rumande.

 “Wasubiri kesho (leo) wataka- poenda mahakamani kama wataamua kuwapa dhamana,” alisema Mambosasa.

Kuhusu baadhi ya watuhumiwa hao kugawanywa katika selo tofauti za Chamwino na wengine kuachwa Kituo Kikuu cha Polisi, Mambosasa alisema huo ni utaratibu wa kawaida ambao unalenga kupata maelezo ya kila mmoja.

“Hayo ni mahojiano tu ili kila mmoja upate anasema nini ndipo unawaweka sehemu tofauti. Hizo ni taratibu za mahojiano ili wasiendelee na mawasiliano,” alisema.

Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi alisema kisheria watuhumiwa hawatakiwi kukaa rumande kwa zaidi ya saa 24.

“Cha kusikitisha siku ya leo (jana) ambayo walisema wangewaleta mahakamani kwa kile wanachoamini wametenda kosa, lakini hadi sasa muda wa mahakama unaisha viongozi wetu hawajaletwa,”alisema na kuongeza:

“Na sisi tunataka kuondoka ili tuone taratibu nyingine ambazo zinaweza kutuhakikishia  usalama wa viongozi wetu. Hadi sasa viongozi wetu hawajaletwa mahakamani.”

Alisema hata kama polisi wanawaona viongozi wao wanamakosa, kisheria hawawezi kukaa na mtu kwa muda wa siku tatu bila kumfikisha mahakamani.

Alisema utendaji wa polisi nchini ni tofauti na wa nje ya nchi ambapo kwa nchi za wengine, polisi ni sehemu ya huduma na si ya mabavu.

 Alisema hali hiyo inaleta kadhia na masumbuko kwa Watanzania na hivyo kupunguza imani yao kwa jeshi hilo.

 Wakili wa watuhumiwa hao, Fred Kalonga alisema wamekuwa na wateja wao tangu siku walipokamatwa kwa kuhakikisha wanahojiwa kwa mujibu wa sheria.

 “Kwa mujibu wa ahadi za polisi kuwa leo (jana) wanaletwa mahakamani. Kuanzia saa 1.30 asubuhi tuko mahakamani na sasa inakwenda saa 9.30 alasiri hakuna mtuhumiwa aliyeletwa. Kimsingi muda wa mahakama umeisha,” alisema.

Alisema yeye na wakili mwenzake, Azack Mwaipopo walikuwa wanakwenda kufuatilia taratibu nyingine za kisheria za kuwawezesha kupata dhamana.

“Tunakwenda kufuatilia taratibu nyingine lakini sisi tupo tayari muda wowote wakiletwa tutawadefend (tutawatetea) kwasababu tunaamini kwa mujibu wa maelezo ya wateja wetu wapo sahihi kuliko tuhuma zinazowakabili,” alisema.

Wanachama wa Chadema walikuwa katika viwanja vya mahakama tangu saa 2.00 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri baada ya kuelezwa na wakili wa watuhumiwa kuwa viongozi wa Bavicha hawatapelekwa mahakamani tena.

Viongozi hao walikamatwa Ijumaa usiku katika baa ya Capetown walipokwenda kunywa na kula chakula. Wanadaiwa kwa tuhuma za kukusudia kuikashfu Serikali.

Akizungumzia mpango wa vijana wa Chadema kuzuia mkutano wa CCM utakaofanyika Julai 23 mjini hapa, Sosopi alisema wanaiheshimu kauli ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ya kuwataka kutokwenda kuzuia mkutano huo.

“Tunaiheshimu kauli ya mwenyekiti na tunatambua kuwa vijana wengi nchi nzima wamejiandaa kwenda kuzuia mkusanyiko huo, lakini sasa tunashughulika na hili la viongozi wetu kukamatwa kwanza,”alisema.

Alisema baada ya viongozi wao kupata dhamana wataitisha kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha haraka ili kujadili suala hilo na watatoa msimamo kama wanakuja na mkakati mwingine ama kuendelea na huohuo
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa vijana wa CHADEMA wanakuwa sio watumishi au wafanya biashara?
    saa ngapi unakuwa na muda huu wakati kuna mambo chungu mzima ya kujitafutia riziki?nyuso ndio hizohizo,sasa mtu unajiuliza kama likizo wanakuwa na siku ngapi za likizo kwa mwaka?Mungu wetu tunakemea hawa wanaowapandikiza vijana wetu na kuwapotosha wakashindwe.

    ReplyDelete
  2. POLENI SANA BAVICHA,MNACHEZESHWA NGOMA MSIOJUA KUICHEZA.
    JIPANGENI UPYA"HAPA KAZI TU"

    ReplyDelete
  3. Lakini TULIA
    Tunaye asifanye bunge kama chuo kikuu alikotoka
    Eti wabunge wa ukawa wamuogope fyuuu
    Chuo wanafunzi walimuogopa atawafelisha mitihani
    Wakati yeye mwenyewe alibebwa na Migiro chuo hadi kubakizwa chuo
    TULIA bunge si chuo
    Unafundisha Yale yake kila mwaka
    Bunge si kukariri kanuni
    Wale ni wabunge wenzeko wanekuzidi
    Hawajateuliwa
    Wamechaguliwa na wanainchi au vyama vyao

    ReplyDelete
  4. We can see your Senior Leadership has changed the Tone and seems now to be patriotic. If what we feel is true.. Then you are welcome to Join us into Transforming our beloved Motherland and Participate fully and Positively into the JPJM march.. Kumukeni kwamba Tanzania itajengwa na Watanzania ambao ni Wazalendo Karibuni sana... Na mkumbuke kwamba Hapa ni Kazi tu na Tunaendelea na Kazi bila kucheleweshwa na hatutaki wacheleweshaji katika kasi Hii.

    ReplyDelete
  5. We can see your Senior Leadership has changed the Tone and seems now to be patriotic. If what we feel is true.. Then you are welcome to Join us into Transforming our beloved Motherland and Participate fully and Positively into the JPJM march.. Kumukeni kwamba Tanzania itajengwa na Watanzania ambao ni Wazalendo Karibuni sana... Na mkumbuke kwamba Hapa ni Kazi tu na Tunaendelea na Kazi bila kucheleweshwa na hatutaki wacheleweshaji katika kasi Hii.

    ReplyDelete
  6. BEBIII... SASA INAKUAJE BEBII.
    TUNAFANYAJE BEBIII... DOLA BEBII NA FARU JONI ANALETA TAHARUKI BEBI

    MBUNGA NAE ANATUNGOJA BEBII NA SACCOZI IMEINGIA HASARA BEBII...

    SASA CHA KUFANYA ..LABDA TUUZE VIMEZA NA TULIPE DENI LA MJENGO..
    WASIJE KUTUONGEZEA MATATIZO NA MWENYE MJENGO WA UFIPA BEBIII.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad