Wafuasi wa Steven Wassira wambwaga Ester Bulaya Mahakamani

Wafuasi wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira wamembwaga mahakamani mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Ester Bulaya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi yao.

Wafuasi hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walifungua kesi ya uchaguzi kupinga ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakijitambulisha kama wapigakura.

Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Mohamed Gwae ilitupilia mbali kesi yao baada ya kukubaliana na pingamizi la wakili wa Bulaya, Tundu Lissu kuwa hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo.

Kutokana na uamuzi huo, walalamikaji hao walikata rufaa Mahakama ya Rufani na wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo waliieleza Mahakama hiyo kupitia kwa wakili wao Yassin Membar kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 111 (1) (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010, wana haki kufungua kesi hiyo.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uzeeeeeeeeeeeeee
    Usingiziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
    Mkoromoooooooooooooooooooo
    Ulopokajiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
    Wasiraaaaaaaaaaaaaaaaaa
    Hunaaaaaaaaassassaa
    Hataaaaaaaaaasaa
    Aibuuuuuuuuu
    Hata kwenye chama hupati cheo ngooooooooooooooiooooooo
    Huendani na kasiiiiiiiiiiiiiiii
    Hapaaasassaaaaaa
    Kasiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
    Tuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad