Zamani ndoa zilikuwa zinadumu sana. Lakini baada ya kuleta haki sawa tu ndoa siku hizi ni miezi miwili ishavunjika. Wanaanza kulala mzungu wa pili, kila mtu anajitegemea kama bachela na hata salamu hawapeani. Haya mambo ya haki sawa yaishie hukohuko Serikalini sio kwenye ndoa zetu.
Wewe unayetaka kuolewa au uliyepo kwenye ndoa, Mheshimu naMsikilize mume wako, Mfundishe, mshauri hata kumuelekeza.
Eti wanawake wa siku hizi wanafurahia kuona mume wake akiosha vyombo baada ya kula, akideki, akifagia, akipika na kubembeleza mtoto alale.
Wanawake wa siku hizi wanafurahi wakiona waume zao wakitangulia nyumbani saa 12 jioni huku mwanamke akija saa tano Usiku.
Wanafurahi kuona anaporudi kwa kuchelewa haulizwi alikuwa wapi, hataki kuona mwaume akigusa simu yake, hataki kupangiwa cha kufanya na mume wake.
Wanawake wa siku hizi wanapenda kuona waume zao wakitandika Vitanda na kuchomekea chandarua ikiwemo kupelekewa maji bafuni. Eti Mwanaume kama unashindwa kufanya hayo, tafuta mdada wa kazi afanye.
Hawa haki sana Wanawadanganya sana. Nia yao wanataka baadae waje wawasimiame katika kugawana vitu baada ya kutandikwa talaka na masikio yake.
Mfano mimi ili unifanyishe hizo kazi, nipe limbwata kwanza. Vingenevyo utaambulia patupu.
Naamini huo sio mpango wa Mungu kunitafutia msaidizi wa kunikalia kichwani. Manaake wanawake wa siku hizi wanajifanya wao ndo kichwa cha nyumba kisa tu Mumefunga ndoa kanisani. Kudadadeki...
By Mdau
Je unakubaliana na Maoni yake?
Toa Maoni yako
Na mtafua sana mtapika sana mtaosha vyombo sana mnapenda mitelezo...kama kazi wote si tunafanya kwan ukinisaidia kuna ubaya gani..kama huna kazi namm mke ndo mwenye kazi basi wewe huna budi kufanya vikazi viwili uwapo nyumban wakt mm.nimeenda kuhangaika na wale wapenda kuopiga wake zaooo weee sio mimi...mm nitakutwanga nduguzo waje wachukue maiti namm nikafungwe..wanaume mmezidi..na mnachosha hasaa....
ReplyDeleteNi kwel huu usawa wanao huzungumzia inawezekana sio mzuri kwenye ndoa,viongozi wa dini ebu tuelimisheni Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi alisemaje kuhusu usawa maana ndoa nyingi zimetawalia na migogoro
ReplyDeleteNdio tatizo la wabongo unaona mke siyo HOUSE GIRL, huyo ni better half. Acha kuwa insecure mwanaume rijali atakaa na kusaidiana na mkewe damnit. Wote mfanye kazi ila yeye ndio umbebeshe majukumu utafikiti ni mama yako mzazi huyo khaaa ndoa mnazivunja wenyeweee wanaume. Siku hizi kwanza ni ushamba kulilia ndoa maana ni utumwa tu na ukimwi juu, heri ukae single na ule maisha.
ReplyDelete