Watu Weusi Waanza Kulipa Kisasi...Polisi watano Wauawa Dallas, Marekani

Maafisa watano wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.

Maafisa wengine sita wanauguza majeraha.
Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha.

Mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema amesema maafisa wa polisi bado wanakabiliana na mshukiwa mmoja ambaye anadaiwa kujibanza katika jumba linalotumiwa kuegesha magari.

“Mshukiwa huyo ambaye tunawasiliana naye amewaambia maafisa wetu kwamba mwisho unakaribia na kwamba ataumiza na kuua wenzetu wengi, akimaanisha maafisa wa usalama na kwamba kuna mabomu yaliyotegwa eneo lote, kwenye gereji na katikati mwa jiji.”

Vyombo vya habari jimbo hilo vinasema kumetokea mlipuko mkubwa eneo hilo lakini habari hizo hazijathibitishwa.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watanzania tujifunze

    ReplyDelete
  2. Weee nawe hapo juu. Watanzania wajifunze nini sasa? Huko Marekani Texas wana yao. Ya ubaguzi wa Rangi hasa Police kuwaonea na kuwanyanyasa watt weusi na mpaka pengine kupelekea kuwawa ndio maana yake ha haya yote, yote hii ni huhasama, huhasama upo wa Aina nyingi, Rangi, dini, Kabira alimradi tu ni ujinga na kutafuta sababu za kunyanyasana na kuwana

    ReplyDelete
  3. We mdau wa pili huna akili hapo mdau wa kwanza anasema wtz tujifunze cos kuna ubaguzi wa vyama hapo tz vilivyopelekea kuuawa wtz kule visiwani+waandishi wa habari wa kwa hiyo wtz tujifunze kwa kweli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna akili mwenyewe. Na hayo mawazo yako. Kila mtu na mawazo yake

      Delete
  4. wewe mwandishi kajifunze wewe

    ReplyDelete
  5. hiyo kabali vipi mwandishi tufafanulie

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad