Wema Afunguka baada ya Kuchoshwa na Majungu ya Watu

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameonesha kuchoka na maneno mbalimbali kutoka kwa watu hususani kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kuamua kutoa yake ya moyoni kwa watu wote ambao wamekuwa wakimfuatilia maisha yake.

Ameonesha kukasirishwa na baadhi ya watu wanaomsema kwenye mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapungufu yake.

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram kuweka ujumbe mrefu kwa watu hao, huku akiwataka wamuache aishi maisha yake kwani hajawahi hata siku moja kwenda kuomba msaada kwao, na kusema hata siku atakapokufa atakufa mwenyewe na kama ni majibu kwa Mungu atajibu mwenyewe.

"Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhalli, sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi. Maisha yangu yananihusu mimi na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, majibu kwa Mungu naenda kujibu peke yangu. Niacheni jamani nimechoka" aliandika Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu amewataka watu ambao wanakereka na aina ya maisha ambayo yeye anaishi waache kuyafuatilia kwani si lazima kufuatilia kile akifanyacho au maisha anayoishi yeye.

 "Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafuatilie siyo lazima. Nisiheme sasa jamanii. Naomba tafadhari kama mapungufu ni ya kwangu mimi. Niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana sipendi kujikasirisha. Kwani nikitajirika mimi au nikiwa masikini wewe unapata faida gani. Jiulize kwanza hilo swali ndiyo uanze kutoa maneno yako" alisema Wema Sepetu

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wema nalia mimi naishi ulaya na hapa wabongo walinifuata sana mama yangu ndiyo wa kwanza baadaye wote pamoja na mama nimewaacha sasa hivi naishi maisha yangu bila mama na bila marafiki maisha yananiendewa sawa hata kama saa nyingine inabidi niongee na watu wa social lakini maisha yananiendewa sawa kuepukana na watu ambao si watu, watu ambao nina waamini ni watu wa social tu

    ReplyDelete
  2. TENA WAKOME KABISA. KILA MTU ANA MAISHA YAKE!! WHY KUMFUATILIA SEPETU???

    ReplyDelete
  3. Na wewe dada acha kuanika habari zako na kutafuta kiki.ukikaa kimya hakuna atakaye kushughulikia.

    ReplyDelete
  4. Umekubali kujiweka public. Ukubali yote. Huwezi cagua. Unaingiza ufahali kupitia public kama hutaki jitoe kabisa.hii ndio faida unayoipata ukianika au kujianika mtandaoni kila siku. Maisha yako yote unafaidi kupitia njia ya mtandao. Watu wasiotaka kuyaanika yao hawajimwagi kwenye mitandao. They are too busy minding their own businesses.hawajianimi hivi. You have no sececracy left .dont you know that. Kila ufanyalo lipo nje. Unachokasirika ni nini.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad