Zambia yakanusha kumzuia Koffi Olomide kufanya maonyesho

Baada ya kuzagaa kwa tetesi ya kuwa Koffi Olomide amekufutiwa maonyesho yake nchini Zambia kutokana na tukio la hivi karibuni la kumpiga dansa wake aitwaye Pamela, Taasisi ya Kilimo na Biashara ya Zambia ambayo ndio waandaaji wa onyesho hilo wamekanusha tetesi hizo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Lusakatimes umeripoti kuwa Taasisi ya Kilimo na Biashara ya Zambia bado inaendelea na maandalizi ya show hiyo.

“Tungependa kuwajulisha wananchi kwa ujumla kuwa mipango maonyesho ya muziki na mfalme wa rhumba Koffi Olomide yaliyopangwa kufanyika tarehe 29, 31 Julai na Agosti 1 bado lipo pale pale. Taarifa ambazo zimezagaa katika vyombo vya habari kwamba Koffi amezuiwa na onyesho limefutwa sio kweli,” taarifa hiyo imesema.

Taarifa iliendelea “Tumesha saini mkataba na Koffi wa kuja na kufanya show katika ukumbi wa Mulungushi International Conference Centre tarehe 29 Julai na zitafuata show za tarehe 31 Julai na 1 Agosti.”

Ijumaa iliyopita akiwa Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, (JKIA) Nairobi, Koffi alinaswa katika video akimpiga teke dansa huyo kwa kilichodaiwa kwamba dansa huyo alikorofishana na mwanamuziki wa kundi hilo aitwaye, Cindy Le Couer ambaye amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Koffi tangu mwaka 2012.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad