Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameunga mkono kauli ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli kuwataka mawaziri wote wahamie Dodoma.
Akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma mapema leo Jumatatu, Rais Magufuli alisema, “Makao makuu yapo Dodoma, Dodoma ndiyo penyewe, haiwezekani wabunge zaidi ya mia saba wanakaa Dodoma na makao makuu ya chama changu ninachokiongoza yapo Dodoma.”
Kauli hiyo inaonekana kupokelewa kwa mikono miwili na Mhe, Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini kwa kusema kuwa uamuzi huo wa rais unapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania.
“Dodoma Kutekelezwa kwa Uamuzi wa kuhamia Dodoma ni sahihi unapaswa kuungwa mkono na Wazalendo wote wa Tanzania,” ameandika Zitto kupitia akaunti yake ya Twitter.
Rais Magufuli anaonekana kukerwa zaidi na viongozi hao wakubwa wa serikali kung’ang’ania Dar es Salaam wakati makao makuu yapo Dodoma na kwa kuonyesha mfano Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza kuhamia mkoani humo mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Dodoma
ReplyDelete