Zitto: Tozo ya Tsh 1000 kwa kadi ya Simu yako kila Mwezi imeanza Rasmi..ni Aibu

Kodi ya tshs 1000 kwa mwezi Kwa kila kadi ya simu uliyonayo imeanza rasmi.

Bunge la wananchi, wawakilishi wa wananchi, limepitisha kodi hii. Hailipwi na kampuni ya simu, inalipwa na Wewe mwenye simu. Kampuni ya simu inakusanya Kwa niaba ya serikali. Ingawa sikuwepo wakati kodi hii inapitishwa na Bunge siwezi kukwepa wajibu wa kuaibika kuwa sehemu ya Bunge hili.

Ni aibu Kwa kuwa pendekezo la kodi hii liliondolewa na Waziri wa Fedha kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato ya Serikali. Pendekezo lilirudishwa namna gani kupitia muswada wa fedha, finance bill, Haieleweki. Ni skandali. Nasikia vibaya sana kuwa mbunge kwenye Bunge lenye maamuzi ya namna hii. Nasikia aibu zaidi kwamba hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo hili.
Ameandika Zitto Kabwe.

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuwa tajiri kwa kuandika blog. Jiunge na matangazo yetu. Bonyeza jina langu hapo ili kujiunga

    ReplyDelete
  2. Tummekussikia tumekupumisha umepomzika. Asante

    ReplyDelete
  3. Ahhhh.. Mbona pesa kuku Tu. Sasa unahilaumu au u atulaumu

    ReplyDelete
  4. Yaani mpaka wewe utuamnie


    ReplyDelete
  5. Elfu moja kwa mwezi mbona ndogo,hata ingekuwa zaidi kwa kuwa lengo ni kusogeza taifa letu pazuri ingekuwa poa tu,tatizo inaumiza hiyo pesa kutafunwa na wajanja wachache.Binafsi kuvuja jasho kwa ajili ya mtanzania mwenzangu kule kijijini au kwa mama zetu wanaozalia chini hainisumbui.Tukemee na kufichua ufisadi kwa nguvu zote.

    ReplyDelete
  6. Hahahaha,
    Akili imeanza kurudi sasa?inaonyesha unajutia kususia bunge,
    umechelewa,hayo ni maamuzi ya waliokuwepo hatuna budi kuyakubali,elfu utakatwa kwa kuwa uko TZ.Eti unasikia vibaya kuwa mbunge kwenye bunge la maamuzi ya namna hii,UNAFIKI mkubwa,mbona hukusikia vibaya kususia bunge?

    ReplyDelete
  7. Si mliona sifa kukimbia bunge,mnavuna mlichopanda.

    ReplyDelete
  8. NASIKIA VIBAYA KUWA NA MBUNGE KAMA ZITO,UMEBEDILIKA SANA.JIUZULU TU,HUJACHELEWA.

    ReplyDelete
  9. Ni aibu ni aibu ni aibu ni aibu kwa mwenye akili za funza ataona sawa tu lakn anayefikiria kwa ndani sana ataona aibu hii...unamkata mwanachi elfu1000 yule wa kijiji asiye na kitu hadi atumiwe pesa na nduguze kutoka mjin yeye atatoa wapi elfu1 ya kila mwezi au asipolipa ndani ya miezi5 atafungiwa lain ya simu acheni mambo yenu....mnatia kichefuchefu haswaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwenda wewe,babako alivyokuwa anafisadi taifa mbona hukuona aibu?

      Delete
  10. Udaku... si mnajua waha wote ni wana uchwara na Hujisemea hovyo hovyo.. Wengine wanakimbia bunge halafu jioni wanapeana habari za upotoshaji ili wazungumze sasa nyie bado tu mnatuletea watu ambao tumesha wa deliti katika fesibuku na tukiwataka tutawafata huko fesibuku na siyo kwenye blog yetu ya udaku... naomba mfupisheni huyu kijeba mleta vioja... Amekwisha pwerewa na wakati.. alikuwa zama zile za utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili sahihi .. lakini si zama hizi zetu hasa katika kipindi cha awamu yetu ya Tano. Hapa kazi Tu. Hawa waliochanganyikiwa akiwa ni mmoja wapo naomba msitupotezee wakati wetu na blog yetu hii mzuri kwa hawa mastelingi na maekta wa filamu iliyokwisha ya Majuziiiiiii!!!!!! Tena ilikuwa senema ya Bule kama wakati wa Cafenol na OMO......Hata Regan ameshakufa

    ReplyDelete
  11. Udaku... si mnajua waha wote ni wana uchwara na Hujisemea hovyo hovyo.. Wengine wanakimbia bunge halafu jioni wanapeana habari za upotoshaji ili wazungumze sasa nyie bado tu mnatuletea watu ambao tumesha wa deliti katika fesibuku na tukiwataka tutawafata huko fesibuku na siyo kwenye blog yetu ya udaku... naomba mfupisheni huyu kijeba mleta vioja... Amekwisha pwerewa na wakati.. alikuwa zama zile za utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili sahihi .. lakini si zama hizi zetu hasa katika kipindi cha awamu yetu ya Tano. Hapa kazi Tu. Hawa waliochanganyikiwa akiwa ni mmoja wapo naomba msitupotezee wakati wetu na blog yetu hii mzuri kwa hawa mastelingi na maekta wa filamu iliyokwisha ya Majuziiiiiii!!!!!! Tena ilikuwa senema ya Bule kama wakati wa Cafenol na OMO......Hata Regan ameshakufa

    ReplyDelete
  12. Yupo yupo Tu. Katila muda WA majeluuhi...Mechi imesha kwisha

    ReplyDelete
  13. Si ndiyo amekurupuka...baada ya kuingia Mitini..Ameshapoteza signo zinagonga mnara.

    ReplyDelete
  14. Demokrasia imechukua Mkondo wake. Vijana wadogo wanshindwa kutumia akili zao Vizuri kufikiri.Kila kinachoonesha mwelekeo wa maendeleo wao wanapinga. Wamefikia kuwasupport Mafisadi Wakuu wa Nchi hii ambao ndo kupe wa maendeleo, Tatizo la Zitto ni kutafuta Umaarufu tu & cheap popularity, kwa sasa amekwama, Mtaani kakwama na Bungeni kakwama.Hata 18% ya miamala walipinga, walijaribu kuwapotosha wananchi, Thanx god TRA wameliona hilo na kupigilia msumari wa moto, Pia wananchi tumewatambua kwamba hawa watu ni wababaisha na wenye Uchu wa Madara tu. Rais wetu JPJM kawaelewa vema sasa amewapiga pini Mikutano yenu ya Upotoshaji sasa Taifa linasonga. Now we can see the light at the end of the turnel
    Keep it up- Sisis Wancnhi tupo nyuma yenu.
    Mtanzania
    From Another Mother

    ReplyDelete
  15. Duh. Huyu kijana anatia huruma. Anatapatapa anatafuta pa kushika. Miti yote imeshateleza.

    ReplyDelete
  16. Nani kamwambia Zitto kuwa fb ndio binge la sheria.Alikimbia mwenyewe bungeni so anyamaze tena kimya kwani upinzani mwaka huu wameligharim taifa letu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad