Zuio la Mikutano ya Kisiasa ni Kumyima Mwanchi Uhuru wa Haki ya Kujumuika- Kijo Bisimba.

Serikali imetakiwa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo zimeonekana kuwa kandamizi ikiwepo ile sheria za vyombo vya habari ambazo zinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wenyewe.

Akitoa ripoti ya nusu mwaka mbele ya wanahabari kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa vyombo vya habari havifanyi kazi kwa uhuru kwani zipo sheria ambazo bado ni kandamizi.

”Vyombo vya habari bado havina uhuru kwani sheria kandamizi bado zinatumika mfano, gazeti la mawio kufungiwa na kutakiwa kutoandika nakala zake hata kwenye mitandao bila sababu maalumu”.Ilielezwa katika ripoti ya kituo hicho

Aidha ripoti hiyo ya miezi sita imesema kuwa wananchi bado wananyimwa haki zao za msingi  ikiwa ni pamoja na  kunyimwa haki ya habari kwasababu  serikali imeamua kutorusha matangazo ya bunge kwa sababu mbalimbali ambazo zinakinzana.

Katika ripoti hiyo pia imegusa haki za kujumuika ambapo kituo hicho kimesema matamko ya jeshi la polisi hasa katika kuzuia mikutano ya vyama imeonekana  kupendelea chama tawala huku vyama vya upinzani  vikiwa vinakandamizwa.

”Mfano mkutano wa Chadema shinyanga ulipewa vibali vyote lakini baadae ukaja kutawanyishwa kwa kutumia nguvu mpaka mabomu, aidha ACT walikuwa na kongamano la kuchambua bajeti lakini jeshi la polisi walizuia lakini wakati huo huo CCM walikubaliwa kufanya mkusanyiko” Ilieleza semu ya ripoti ya Kijo Bisimba.

Pamoja na hayo ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa Serikali  ikiwa kuboresha sheria hizo kandamizi kwa wananchi pamoja na kuachia vyombo vya habari kufanya kazi zake pasipo kuingiliwa sambamba na Vyama vya siasa kupewa haki sawa.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi sijaelewa.. Serikali imetakiwa kufanya Marekebisho na NANI?? Inzungumziwa ripoti !! Ripoti gani na Muandika Ripoti ana sifa Zipi na kumwezesha kuifanya hiyo inayodaiwa kuwa ni ripoti!! na ametumwa na nani au ameombwa na nani?

    Pia nashindwa kuelewa muhimili wa huyu anayedai ripoti kuwa Biased to an extende yeye ameona kuwa kutorusha bunge live kumemnyima mwananchi haki,, ajili ya live japo anapata habari katika kipindi maalumu cha leo bungeni na Redioni..

    Nikingoja majibu napenda kusema,, This is Baseless and Biase to affiliation to certain Party whereby it make the so called report as a Garbage with the intention of satisfying certain group and individuals in general Its unproffesional..and the right word should be Suggested rather than imetakiwa.. Tanzania ni nchi na ina heshima yake na watu wake na viongozi wake,,, Sasa wewe kama ni mwanachama na una sera za kuingiza chama chako... Tunakwambia Jipange tena. Hii Suggestion yako imegonga Mwamba hapa... Hapa ni Kazi tu.. na sijui umeiwasiliwa mahali manake sijaiona!!!

    ReplyDelete
  2. Hawa watu wa haki za binadamu mara nyingi wanajitokeza kwenye mambo ya kisiasa zaidi, hasa hasa wanaegemea upande wa upinzani hasa chadema, sijui kwa vile wengi wao ni wachaga?? Kweli kabisa siwaelewi hawa watu! Kuna watoto na watu wengi wananyanyasika huwasikii wakizungumza wala kufuatialia, wamekalia siasa, siasa na maandamano, yaani wanapenda vurugu kuliko amani hawa watu...SIWAPENDI SIWAPENDI SIWAPENDI..... WAMESHINDWA NA WAMESHALEGEA!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad