Nikiwa BOLE nikisubiri connection ya karibu masaa sita,nikashuhudia moja ya ndege za Ethiopia zilizopachikwa jina la "The Mount Kilimanjaro".Nikakumbuka kuliwahi kuwa na mjadala mkubwa sana kuwa Kenya kwa kutumia ndege yao aina ya Boeing777 wanautangaza mlima Kilimanjaro na kuonyesha kama upo kwao na si Tanzania.Mjadala huo uliwahi kufika bungeni ukichagizwa na Mama Anna Kilango wakati huo akiwa mbunge wa Same Mashariki.Wakati sisi tukilala,wenzetu wanatumia fursa za vivutio vyetu kujinadi
Nilipoona na Ethiopia Airways wametumia jina la "Mount Kilimanjaro" nikataka kudadisi,je na wao wanasadikisha huo mlima upo Ethiopia?Lkn jibu nililopata ni kuwa wao wameandika ili kuwaonyesha watalii mbalimbali duniani wanaopenda kuja kuutazama mlima huo kuwa unaweza kufika Kilimanjaro kwa kupanda Ethiopia Airways kupitia Addis Ababa hadi KIA,na ndio maana wao hupenda kuipeleka ndege hiyo kwa "route" za KIA na BOLE.
Ethiopian Air line |
Mlima wetu unatangazwa na mataifa mengine,tuombee nia ya Rais kuifufua ATCL ili na sisi tutumie ndege zetu kuutangaza mlima wetu na vivutio vingine vya utalii,Kwani KQ wana ndege wamezipa jina la "Maasai Mara","Serengeti","Ngorongoro" nk.We are waiting for you dear ATCL.
Watanzania kujituma au kutojituma akutoi ruhusa Kwa walio siwaatanzania kutumia logo zao, hao unadai wanatumia fulsa basi ni lazima waombe hiyo fulsa Kwa wahusika, kulaumu watanzania hakukufanyi uwe smart bali stupid
ReplyDelete