Agizo la Rais la Kugawia Wananchi Mawe ya Dhahabu laanza Kutekelezwa Mgodi wa Geita

Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Geita la kuwagawia wananchi mabaki ya mawe maarufu kama Magwangala kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita GGM umeanza kutekelezwa.

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo yupo katika ziara ya kikazi katika mgodi huo kwa kutafuta sehemu ambayo wachimbaji watayaweka na kuyachenjua kwa ajili ya kuyagawa kwa wananchi.

Akiongea mara baada ya ziara hiyo Mhe. Muhongo amesema kuwa agizo la Rais lilikuwa ni baada ya wiki tatu lakini kwa kuwajali wananchi wa eneo hilo wameamua kuanza zoezi hilo mapema kwa ajili ya utekelezaji wa agizo la rais.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Emanuel Kiunga, amesema kuwa serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wabunge wa mkoa huo na baadhi ya viongozi wametafuta maeneo ya kuweka Magwangala hayo kwa ajili ya kuyahifadhi.

Wakizungumzia maeneo hayo yaliyotengwa kwa ajili ya zoezi hilo baadhi ya wabunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa viti Maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Upendo Peneza, na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma wamesema serikali lazima iwe makini na mawe hayo pamoja na kuwajali wananchi wa maeneo yaliyotengwa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hayo mawe magwangala soko lake ni wapi? yanauzwa wapi yaani?! kwa nini msiwape dhahabu au dhahabu ya wazungu?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad