Augustino Mrema: Mimi ni mpinzani mstaarabu

Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Mrema amewaonya wapinzani wenzake kuacha kupanga kufanya maandamano Septemba, 1 na watumie muda wao kushirikiana na Rais Magufuli kufanya kazi ili kuleta maendeleo kwa watanzania.

Mrema ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm na kusema kuwa wanatakiwa kufanya siasa kama anayoifanya yeye ya kuwa mpinzani mstaarabu ambaye anaunga mkono kazi zinazofanywa na Rais Magufuli.

“Mimi ni mpinzani mstaarabu, upinzani wa kijinga siutaki kama wewe ni mpinzani wa kweli inatakiwa ukae bungeni ili kutoa matatizo ya watanzania lakini sasa wao wanatoka ningekuwa mimi nisingetoka, niwashauri tu wakae wafanye kazi,” alisema Mrema.

Aidha Mrema aliwaonya Chadema kuacha kupanga kufanya maandamano ya UKUTA kwani rais wa sasa ana nia ya dhati kuwafanyia kazi watanzania na kama wamekosa kazi ya kufanya waende shambani kulima au kusaidia kutatua tatizo la madawati.

“Rais ameshasema apewe muda kuleta maendeleo kwa watanzania na yeye ndiyo mwenye majeshi kama wamepanga kufanya maandamano wasidhani kitawakuta kama kilichonikuta mimi mwaka 1995, rais anataka tu kazi kama hawana ya kufanya waende mashambani kulima au wakatafute madawati,” alisema Mrema.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MREMA PITIA HAPO KWA MANGI UPATE MTORI BABANGU.TUNAPENDA WANASIASA KAMA NYIE,SIO HAO WA MAPOVUUUUUUUUUUUU KWA KILA KITU.WATUACHEE!

    ReplyDelete
  2. Hahahahah!wakuulize wewe tuliyekupenda kupita wote waliowahi kugombea urais kwa upande wa wapinzani,na amani bado inatawala.

    ReplyDelete
  3. Tatizo CHADEMA hawana wazee wa busara wa kuwashauri.

    ReplyDelete
  4. KANDAMIZA MREMA.

    ReplyDelete
  5. Mrema...tofayti yako Na Wao..ni kwamba wewe unaelewa Na Ni mchapa kazi Na huiogopi kazi..wao Ni waoga ya kazi katila kipindi cha HAPA KAZI TU..Chini ya Bab JPJM..na waneamua kumpa ushirikiano fintu katila ujenzi. WA taiga letu..Na sisi tumeamua kuwapa mapumziko ya muda mrefu ambacho ndicho wanachokipenda baada ya kuogopa kazi wakati WA kuufanya Kazi Na hv wako misheni town kuanzisha uvurugaji WA WA Kazi kwa ukuta Na sisi tuneshaweka magreda kuanza kazi..Hongera Mrema kwa Uzalendo wako

    ReplyDelete
  6. Waambie tu baba usichoke,
    Wanajifanya hawaelewi wakati kazi wameanza kuiona.

    ReplyDelete
  7. Wachangiaji wote hapo ni wapumbavu
    Na wajinga wasiojuwa maendeleo kwanini
    Ulaya magharibi na USA
    Wameendelea
    Chama hakuwezi kutawaza 50
    Years
    Ujinga huuuuuuu

    ReplyDelete
  8. Mstaraabu au njaa inakusumbua?mbona ulivyokuwa mbunge hukusema?unazeeka vibaya sana.

    ReplyDelete
  9. Mzee Mrema: Rais alikuwahidi kazi na kweli amekupatia kazi!! Sasa chapa kazi uliyokuwa unaiomba. Ombi langu ni ili magareza mengi kuna watu waliofungwa kwa kusingiziwa tu!! Ni wengi sana wewe unalijua hilo na pia mtukufu rais anafaham kabisa kuwa wafungwa wengi,wamefungwa kutokana na rushwa za mahakimu, majaji,polisi na watu wengi wasio muogopa Mungu.Nakuomba shughulika na wafungwa ambao wamefungwa kwa sababu za sintofahamu. Mungu akubariki,Mungu ambariki rais wetu na Tanzania.
    JB USA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad