MBOWE :-CHADEMA TUTAUNGANISHA NGUVU NA ACT WAZALENDO KUPINGA UDIKTETA.
Waswahili walisema usitukane Mamba ujavuka mto, msema huo waelekea kutimia kwa Freeman Mbowe na cdm yake kufuatia kudorora kwa mpango wao wa Ukuta sasa akimbilia kuomba msaada wa Zitto Kabwe na chama cha ACT Wazalendo.
"Hatuwezi Kukaribisha Watu Kama Mrema Au Cheyo Ambo Vyama Vyao Vimeamua Kushirikiana Na CCM, Tutazungumza Na ACT WAZALENDO Tulioshirikiana Bungeni, Wameonyesha Kuwa Wanapingana Na Udikteta Kwa Hivyo Milango Ipo Wazi Kwa Sisi Kuungana Nao (WAZALENDO) Kuunganisha Nguvu Za Vyama Vyetu"
Amenukuliwa Mbowe Na Gazeti la Citizen
Nini maoni yako? .sasa wale walo karirishwa eti Zitto Kabwe ana tumiwa na ccm, mamluki, anataka kuoa kwa kikwete. Awaaulize chadema kwa nini waliwadanganya? Maana leo zitto na ACT WAZALENDO wanaonekana wapinzani wa kweli, na sio ccm tena. Siku zote uongo huwa haudumu. Mtaendelea kuumbuka tu.
(MUNGU HAMTUPI MTU MWENYE DHAMIRA YA KWELI. HAWEZI SHINDWA WALA HAWEZI KATA TAMAA) Na bado
WEWE MWANDISHI UMETUMWA, NA WALIOKUTUMA NI HAO CHAMA CHA MAZINGAOMBWE. HESHIMU CHADEMA HESHIMU ACT.
ReplyDeletembowe. Zito usifikiri ni mwenzako..uliyomfanyia anayakumbuka na anayajua.?!!na unyama wako hajausahau na wala hatousahau..tuwachie chama chetu na zito..
ReplyDeleteMh Zito ni kijana makini sana na ni tegemeo kubwa kwa mustakabali wa demokrasia na maendeleo ya kisiasa hapa kwetu. Tulipo sikia sisi wananchi kwamba ameondoka CDM na kuanzisha chama kipya, sisi mashabiki wake tulifurahi sana. Nadhani hakuna yeyote ambaye anaweza kumrubuni Zito anawajua ndani nje. Mh Zito songa kivyako nuru inakuwakia mbele yako achana nao hao hawana jipya.Kesha kunywa maji huyo ana tapatapa na mikakati hewa anatafuta wa kuzama naye. ACT peke yenu ndiyo chaguo letu la upinzani wa kweli msihadaike.
ReplyDelete