Dk. Tulia Afunguka, Asema Ukawa Walimtukana Tusi Kubwa

SIKU mbili baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuahidi kufanyika maridhiano kati ya uongozi wa Bunge na wabunge wa upinzani katika kikao kijacho kinachotarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amesema hataki kuwasikia wabunge wa upinzani wala kuwawaza.

Kauli hiyo ya Naibu Spika huenda ikazidi kutonesha kidonda hasa baada ya Bunge la Bajeti lililofanyika Mei mwaka huu kuacha majeraha kutokana na wabunge wa upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia vikao vyote vilivyoendeshwa na kiongozi huyo.

Juzi wakati akihojiwa kupitia kipindi cha Funguka kinachorushwa na Kituo cha Luninga cha Azam, Spika Ndugai,  alisema anatafuta mbinu ya kuweka sawa mambo hayo kwa kufanya maridhiano  ikiwemo kushirisha maspika wastaafu.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania juzi katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Tulia alisema hapendi kuwawazia wabunge hao wa upinzani.

“Kwa kuwa Spika yeye kazungumza siwezi kucomment chochote kwa sababu sipendi kuwawazia wabunge hao,”alisema.

Alipoulizwa kwamba ni kwanini migogoro ilizidi wakati yeye akiwa anaendesha vikao, alisema alichokuwa anafuata ni kanuni na kwamba malalamiko hayawezi kukosekana.

“Nashangaa wengine wanasema kuendesha vikao ni mpaka uwe na uzoefu…unajua zile kanuni hata ukipewa uendeshe wewe ukishazielewa hazihitaji uzoefu wowote. Kulalamika kuwa nawapendelea ni jambo la kawaida.

“Kwa mfano siku iliyotokea vurugu wakati wabunge wa upinzani wanadai kutorushwa matangazo ya Bunge live, aliyekuwepo kwenye kiti alikuwa ni mwenyekiti ambaye ni mzoefu wa siku nyingi na ni yeye aliyepeleka majina yao kwenye Kamati ya Maadili, sasa sidhani kama hiyo ni hoja,”alisema Dk. Tulia

Alieleza kushangazwa kwa kitendo cha wabunge wa upinzani katika barua yao waliyomwandikia Spika kwamba hawana imani naye, huku akihusishwa na fedha zilizorejeshwa serikalini.

“Katika ile barua walieleza sababu nyingine kuwa hawana imani na mimi, wakanihusisha na zile Shilingi bilioni 6 zilizorejeshwa serikalini wakati sheria na utaratibu upo wazi kwa sababu Spika au Naibu Spika hauhisiki na masuala ya fedha bali anayehusika ni Katibu wa Bunge.

“Kwa hiyo ni jambo la kushangaza kwamba Naibu Spika karudisha fedha, mimi si mshika mafungu lakini pia ni namna watu walivyopokea huwezi kuwazuia wanavyokuwazia,” alisema.

Akizungumzia kauli ya Spika Ndugai kwamba kwa kuwa Bunge la 11 lina wabunge wapya wengi na kwamba kuwaongoza kunahitaji uvumilivu mkubwa alisema: “Nisingependa kuongelea kauli ya Spika…lakini uvumilivu wa mtu kutakiwa akae hadi mara 11 halafu ameendelea kusimama ni uvumilivu gani huo?,” alihoji.

Pamoja na mambo mengine alisema wakati wabunge wanawake wa Ukawa walipojitoa kwenye  Chama cha Wabunge Wanawake (TWPG), alitukanwa tusi kubwa lakini alinyamaza.

Mei 5, mwaka huu wakati akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, Mbunge wa Ulanga Mashariki, Gudluck Mlinga (CCM), alidai kuwa ili kuwa mbunge wa viti maalumu Chadema lazima uwe ‘baby’ wa mtu.

“Laiti ungeona Hansard tusi walilonitukana siku ile, actually Mlinga hajatukana lakini ulisikia nikilalamika mahali kwamba nimetukanwa? wao wanaongee vibaya…watukane, mimi bado ni kiongozi wao na siwezi kuanza kuwakasirikia itakuwa sasa nashindwa kuwaongoza mimi ni kama mzazi wao,” alisema Dk. Tulia.

Alisema kitendo cha watu kudai kwamba anafanya upendeleo bungeni ni changamoto ya kawaida, kwa sababu hata katika mabunge ya Jumuiya ya Madola malalamiko ya aina hiyo yapo.

“Pale bungeni  wako wabunge 389, hawa ni wengi sana wote hawawezi kupata nafasi ya kuongea. Kwa mfano uliomba nafasi jana ukapewa ukaomba leo, hata ukisimama mara 11 katika hali ya kawaida huwezi kupewa kwa sababu wako wengi ambao hawajachangia.

“Kama kiongozi naona ni sehemu mojawapo ya kusimamia jamii ni changamoto na itaendelea kuwepo kwa miaka mitano,”alisema Dk. Tulia.
Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tulia koma wewe bunge si chuo kikuu ambako Mgiro alikubeba na kukubakisha chuo
    Wabunge si wanafunzi Kama wa chuo wakuogope utawafelisha mitihani
    Japokuwa wewe mwenyewe ulibebwa na Migiro ukabakia chuo
    Hata kuzaa ulizalia kwa Migiro USA wakati akiwa naibu katibu Mkuu wa UN
    Eti unatamba umechaguliwa na na rais
    Kweli wewe u kilaza Kabisa kuna hadhi na tofauti ya wabunge
    Majimbo it's like president ktk majimbo
    The rest ni wabunge wasiokuwa na mshiko
    Usijifananishe Kabisa
    Unaibu spika hufai
    Sisi watoto wa kike toka uni Dodoma hatutokusahau maishani
    Tupo tuliopata
    Ukimwi
    Mimba
    Kurepiwa
    Kwa sababu yako wewe Mwanamke usiyejuwa wala kuona huruma kwa binadamu wenzako
    Uliona bora uwafukuze wabunge wa upinzani kulikoni kujadili hoja yetu wanafunzi 7000
    Mungu atatulipia
    Amen

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe anony 4:31 PM hebu tutolee shombo una mdomo mchafu kama ulivyo mwenyewe unaonekana una tatizo lako binafsi na Tulia ni kubwa kuliko hata tatizo la UKAWA na Tulia

      Delete
    2. We ni mpumbavu, kweli wwe ni kilaza. Na ndo maana ulitimuliwa, bado hujaelewa sababu za kufukuzwa chuo?

      Delete
    3. Washenzi nyie tukianika mengi hapa patakuwa hapatoshi
      Tunajuwa in and out
      Anafaa kuwa mtendaji
      Ushauri wa bure

      Delete
  2. Mtoa hoja kama uliyoyasema yana ukweli hapo kazi ipo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli abishe hapa
      Tuanike yote na ushahidi tosha
      Asijitie kujuwa sana

      Delete
  3. TULIA wewe mzazi wa Nani
    Labda hao wabunge wa CCM hata huko kuna watu hawskupendi
    Umeingia na vishindo bungeni
    Makinda alitoka mbali
    Hatukatai Kama ungekuwa unafuata kanuni au miongozo kwa wabunge wa CCM pia
    Fyuuuuuuuu
    U bado kinda CCM wamefanya makosa kukupa cheo hiki
    Hata wao wanajuta
    Hehe mita 200 mchezo

    ReplyDelete
    Replies
    1. unaongea pumba tupu we anony 10.25pm kajifunze kuandika usituletee shombo zako mjinga wewe

      Delete
  4. Kumbe imeuma. Hapa hatutaki kusikia the past kwakua hatujui yako weka jina we mtoa comment wa kwanza kama kweli una ubora ndio wale wale ngwa ngwa ngwa ze chea hadithi simulizi mko wengi sana pole hapa kazii kwa kwenda mbele. Usibanie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vijibaby fyuuuuuuu
      Tanzania haiendeshwi kwa nguvu
      Fyuuuuu
      Kikwapa
      Cha loleza na zanaki

      Delete
    2. Niweke jina nitekwe
      Na yeye kisha sema ni mbunge bora kuliko wote kateuliwa na rais wa kwanza kuteuliwa
      Kaka Lisu Kesha sema mahabusu si kuzuri
      Lakini jafari kuwa naibu wala spika

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad