Hirizi ya Tiffah yaibua jipya!

Mtoto wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote Agosti 3, mwaka huu ametimiza mwaka mmoja lakini jipya lililoibuka ni kuhusiana na dawa ‘hirizi’ aliyovalishwa mkononi na bibi yake mzaa baba, Sanura Kassim ‘Sandra’, Risasi limenyetishiwa ubuyu.

Chanzo kutoka ndani ya familia ya mastaa hao kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, awali Tiffah alivishwa dawa hiyo lengo likiwa ni kumkinga na matatizo lakini Zari alipokwenda Sauzi akamvua kwa kuwa yeye si ‘muumini’ wa mambo hayo.

tiffaIkadaiwa kuwa, baada ya Zari kumvua walikaa muda mrefu bila Tiffah kuwa na ‘kadawa’ hako hali iliyomfanya mtoto huyo achelewe kutembea.

“Unajua ile dawa ina mambo mengi kwa watoto, inamsaidia kumkinga na matatizo lakini pia inamfanya atembee haraka, sasa walipoivua ikamfanya achelewe kutembea,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:

“Hali hiyo ilisababisha Zari na Diamond kutofautiana na mwisho wakakubaliana hirizi irejeshwe mkononi mwa Tiffah ndipo mtoto huyo alipoanza kutembea.”

Ikaelezwa kuwa, kuanza kutembea kwa Tiffah kumeibua furaha upya kwenye familia hiyo kwani walishaanza kuwa na hofu hasa ikichukuliwa kuwa, Zari ana mimba nyingine na anatarajiwa kujifungua Desemba, mwaka huu.

Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Diamond na alipopatikana alisema kuwa ni kweli mtoto wao ameanza kutembea lakini si kwa sababu ya dawa hiyo aliyofungwa mkononi.

“Hayo mambo ya kumvalisha na kumvua Tiffah ile dawa ya mkononi ni uamuzi tu lakini huwezi kusema ina uhusiano na kutembea kwake,” alisema Diamond.

Source:GPL

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inawahusu muacheni malaika wa watu na Bangili yake nyeusi,,,watoto wangapi wanazo mpaka shingoni chaa ajabu nini,,,utamaduni wao.

    ReplyDelete
  2. Uyo anaeita hirizi yeye aijui au ajavaaa au anajishaua tu

    ReplyDelete
  3. Mila mila hata kama ni upuuzi basi ili mradi ni mila tu mambo ya kuvalishana iwe hirizi kamba ukindu au waya ni mambo yaliyopitwa na wakati eti bila hirizi mtoto hasingeweza kutembea au amechelewa kutembea fuh!Mwalimu wangu wa biology wakati nipo shuleni hakunifundisha hivyo eti myoto akizaliwa nimvishe hirizi mkononi ili aweze kutembea whatta bullshit watoto wangapi bongo wakizaliwa kila mtoto tupo tofauti kiukuwaji mwingine anakuwa mwepesi meingine anachukua muda lakini mwshoni wote watatambaa kutembea na kuanza kusema hiyo ni asili ya mwanadamu na si vinginevyo na mila za kishenzi ndiyo maana hatuendelei karne zimeenda lakini wengi wetu bado tupo kimawazo na kimatendo kwenye zile karne za stone age ndiyo maana hao waganga wa kienyeji huwa hawalali na njaa maana watu wanaoamini hivyo wapo wengi badilikeni nendeni na wakati

    ReplyDelete
  4. Angalia huyo hapo juu anavyosema kuwa mtoto Tiffah ni Mmanyema yale yale ya mila na fucking desturi aliyemzaa mtoto ni mama baadaye mtoto anakuwa ni mali ya baba atapewa jina la baba atachukua dini ya baba atachukua kabila ya baba na atakuwa mali ya baba hapo mama hana chake kabisa wakati yeye ndiye aliyemzaa mtoto huyo kwa uchungu kumtunza na ghasia zote baba yeye yupo pembeni tu lakini juu ya kazi zote hizo alizozifanya mama bado hana haki kwa mtoto wake kimila mwenye haki ni baba je hamuoni kuwa hapo pana walakini?

    ReplyDelete
  5. Kama wewe utaki kitu basi haikupi haki ya kutukana na kukataza wengine wewe fuata biology na huyu asietaka mila anzisha mila yako au fuata mabwana zako wa ulaya, na wanaotaka kufuata mila za kimanyema basi nyema nyema kama Kawa lol

    ReplyDelete
  6. Mtoto yyte akizaliwa anakuwa tayari anayo dini, mtoto anatoka kwenye dini yake aliyozaliwa nayo pale baba au mama anapompeleka kubatizwa au kufanyiwa utaritibu uliopangwa na wanaadamu, hivyo Tiffany afuati dini ya baba yake bali dini anayo toka alipozaliwa kuhusu kabila hayo ni matakwa ya wazazi kukubaliana sio unayoyasema ni uzushi na propaganda za wasiopenda watu kujiamulia mambo wenyewe Tiffany ni rahisi kuzungumza na kufuata lugha na kabila la mama kabla ya baba

    ReplyDelete
  7. Bado giza tupu machoni mpaka karne hii

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad