Jeshi la Polisi: Mazoezi Yanayoendelea ni ya Kawaida, Hayalengi Kuzuia Shughuli zozote Halali

Taarifa ya Jeshi la Polisi Kwa Vyombo Vya Habari

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi

Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli Amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga
    Tanzania imekuwa hivi??????
    Amwamu zote zimepita hatukuwa hivi
    Tatizo nini haswa
    Mnatisha Nani
    Mazoezi
    Watanzania naona sasa tufungue macho yetu
    Asiyependa kukosolewa si kiongozi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad