Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, limeendelea na mazoezi yake kwaajili ya ukakamavu ili kujiweka sawa na kupambana na tatizo la uhalifu.
Akiezungumza na waandishi wa habari Kamishna wa polisi kanda ya Dar es salaam, Simon Siro, aliwatoa hofu wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi na zoezi hilo kwani halipo kwaajili ya kuwatisha bali lengo ni kupambana na wahalifu na majambazi.
“Eeh kimsingi ni mazoezi ambayo tunayafanya kupitia maeneo mbalimbali kwa maana kwamba lengo kubwa ni kuzuia uhalifu hilo ndo lengo la kwanza, la pili ni kupambana na uhalifu kwasababu tunapokuwa tunapita maeneo mbalimbali lolote linaweza kujitokeza, wahalifu wanaweza jitokeza”, alisema kamanda Siro.
Aliongeza kwa kutoa mfano wa matukio yaliowahi kutokea alisema, “matukio mengi unaweza kuona kama ya panya rodi yanatokea sana sana maeneo ya Mbagala, lakini tukaona kwanini tufanye mazoezi haya kimya kimya ni vizuri wananchi wa kaona jeshi lao wakaona ukakamavu wa askari wao.”
“Hata miaka ya nyuma tulikuwa tunafanya na wala hatuna nia mbaya kabisa kwamba tunatisha wananchi hapana hatuna lengo la kutisha tunafanya katika mazoezi yetu ya kawaida na lengo kubwa kuzuia uharifu kwenye maeneo kwasababu naamini mtu muharifu akiona polisi anapita anakimbia”, aliongeza .
Naye kamishna wa oparesheni wa mafunzo ya jeshi la polisi Nsato Nsazya, aliwataka wananchi wasikejeli mazoezi hayo na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya hivyo kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia mitandao ya kijamii.
Sijwahi sikia wala kuona dunia nzima eti polisi wakafanya mazoezi kwenye maeneo ya raia
ReplyDeleteTanzania tumeendelea kweli
Kwani hawana mafunzo vituoni
Hongereni kwa intelinjisia bora duniani!!!!!!!!???
Mazoezi tunayoyajuwa dunia nzima ni mazoezi ya maafa, moto,
ReplyDeleteMafuruko , hospital nk
Haya hufanywa kwenye maeneo ya raia
Lakini si ya kejeshi
Naona mna lenu Jambo
Mungu ibariki Tanzania
Fyuuuuuuu
ReplyDeleteTangu lini ukamuonesha mhalifu au Adui utakavyo mkabiri
Kwa kumuonesha silaha au njia gani utumiazo
Kweli polisi wa bongo vilaza Kabisa
Kwa kuwasha maji na mabomu ya machozi
Adui akivaa musk na bullet proof utampata
Nasikia kutapika
Siro nawe u jipu
ReplyDeleteBora jitumbuwe kabla hujatumbuliwa
Kwani umekuwa msemaji wa jeshi la polisi
Wewe ni Kamanda
Fyuu rudi shule
Tumekuchoka kwenye media
Fyuuuuuuhhhhh
Hata huyo bosi wako mkuu wa jeshi la polisi haonekani mitaandao au media Kama wewe una Fanya kazi saa ngapi
?
Au unapiga doria mkuu masaa 24 ?????????
Jeshi letu ni Imara na Zuri zana. Makamand wetu na vijana wetu wako sawa kabisa katika jukumu lao la kutulinda sisi Rais na Mali zetu. Fikira na mwonekano ni Mzuri na Imetujengea Imani kwamba Amani tunayo na Itaendelea kuwepo. Sasa nyie mnaotaka kutujaribu mjue kabisa kwamba mkijaribu hatutosita kukushughulikieni. fanyeni kazi mjenge taifa na kuleta maendeleo. Ukijaribu tutacheza na wewe.. Hapa Kazi Tu. Hongera wana Usalama wetu na Majeshi yetu imara na Makachero wetu. Tunaaminini tuko katika Mikono Salama. chini ya Baba JPJM. Mungu akubarikini na kukulindeni wote na adumishe Amani na Utulivu nchini kwetu. Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
ReplyDeleteJeshi letu ni Imara na Zuri zana. Makamand wetu na vijana wetu wako sawa kabisa katika jukumu lao la kutulinda sisi Rais na Mali zetu. Fikira na mwonekano ni Mzuri na Imetujengea Imani kwamba Amani tunayo na Itaendelea kuwepo. Sasa nyie mnaotaka kutujaribu mjue kabisa kwamba mkijaribu hatutosita kukushughulikieni. fanyeni kazi mjenge taifa na kuleta maendeleo. Ukijaribu tutacheza na wewe.. Hapa Kazi Tu. Hongera wana Usalama wetu na Majeshi yetu imara na Makachero wetu. Tunaaminini tuko katika Mikono Salama. chini ya Baba JPJM. Mungu akubarikini na kukulindeni wote na adumishe Amani na Utulivu nchini kwetu. Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
ReplyDelete