Jukwaa la Wahariri lapinga Mseto kufungiwa

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepinga hatua ya Serikali kulifungia gazeti la Mseto kwa mtindo wa yenyewe kujifanya mlalamikaji, mwendesha mashtaka na hakimu.

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa mshituko taarifa za kufungiwa kwa miezi 36 gazeti la Mseto kwa kutumia kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976.

Katika maelezo ya Waziri, Nape Nnauye anasema tangu Mwaka 2012 wamekuwa wakiwaonya Mseto bila gazeti hilo kubadilika.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Halihalisi, Saed Kubenea amekana kupata maonyo kutoka Serikalini.

Sisi TEF tunapinga utaratibu wa Serikali kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka na Hakimu katika kesi inazohusika.

Tunataka mchakato wa kubadili Sheria ikaanzisha chombo cha kitaaluma cha kusimamia wanahabari na vyombo vya habari uende haraka kwa nia ya kumaliza kadhia hii.

Serikali imeahidi muda mrefu kubadili Sheria hii mbaya ya Magazeti lakini miaka yote utekelezaji umekuwa sifuri.

Tunasisitiza kuwa hatukubaliani na wala hatuungi mkono utaratibu huu wa Serikali kufungia au kufuta vyombo vya Habari.

Kwa upande mwingine tunapenda kuvitahadharisha vyombo vya Habari katika matumizi ya nyaraka ili kuepuka kuingia katika migogoro na Serikali, Jamii au mtu mmoja mmoja.

Pamoja na taarifa hii, TEF itafanya uchunguzi na uchambuzi wa adhabu iliyotolewa kwa Gazeti la Mseto pamoja na habari iliyosababisha gazeti hilo kufungiwa, kwa manufaa ya waandishi wa habari na vyumba vya habari.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo lenu hamna umoja kama mliokuwa nao kwenye kifo cha Mwangosi!! mngekuwa na umoja mambo yote hayo yangekwisha kama mngekubaliana wote kwamba hakuna kuandika habari za serikali mpaka warekebishe baadhi ya mambo yanayo wafanya mfanye kazi zenu kwa wasiwasi na kusua sua nafikiri wangefikia muafaka na nyinyi tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad