Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa Akamatwa Akituhumiwa Kufanya Uchochezi Kwa Kutumia Mitandao ya Kijamii

Wakati Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akiwa nje kwa dhamana baada ya kupandishwa kizimbani kwa makosa matatu yakiwamo ya uchochezi, Jeshi la polisi mkoani Geita limevamia Hoteli ya KG iliyopo mjini Geita aliyokuwa amefikia Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Miku na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Geita, Neema Chazaile na kuwashikilia kwa tuhuma za uchochezi wa kutumia mitandao ya kijamii.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa uongozi wa Chadema Mkoa wa Geita na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa, Mponjoli Mwabulambo zimedai kuwa katibu huyo alikamatwa jana saa 12 asubuhi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Geita, Sudy Mtanyagala alidai kwamba askari wa polisi zaidi ya 10 wakiongozwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa (RCO) waliizunguka hoteli aliyokuwa amelala katibu huyo wakidai wanatafuta majambazi yenye silaha.

 Mtanyagala alidai kuwa polisi hao waliingia chumba baada ya chumba na walipofika katika chumba cha mwisho ambacho ndicho alichokuwa amelala katibu huyo walimkamata na kuchukua simu yake.

Alisema baada ya kumkamata walisoma nyaraka za chama alizokuwa nazo kisha kumtaka yeye na mwenyekiti wa Bavicha kuongozana na polisi hadi kituoni kwa uchunguzi zaidi.

 Alisema katibu huyo wa kanda pamoja na mwenyekiti wa Bavicha mkoa walikuwa wakijiandaa kwa kwenda katika ziara Wilaya ya Nyang’wale ambako wangefanya mikutano ya ndani na viongozi wa chama hicho.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Geita, Hellena Thobias alisema walipata taarifa za kukamatwa kwa viongozi hao asubuhi na kufika polisi.

Alisema baada ya kufika polisi, maelezo yalibadilika na kuelezwa katibu wao anatuhumiwa kwa uchochezi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Alisema wamejitahidi kuomba dhamana lakini imeshindikana baada ya kuelezwa kuwa watuhumiwa hao watakuwa chini ya uangalizi wa polisi kwa uchunguzi zaidi.

“Polisi wametunyima dhamana hadi saa 10 jioni tuko polisi tumeomba dhamana wamekataa sijui ni sheria gani inayomzuia mtu kupata dhamana lakini pia sijui ni sheria gani ya polisi kumnyang’anya mtu simu yake bila ridhaa na kuichunguza. Hatutanyamaza juu ya uonevu huu,” alisema.

Alisema Serikali imekataza mikutano  ya hadhara na kueleza kusikitishwa kwake na hatua ya jeshi la polisi kufuatilia hadi mikutano ya ndani ya chama hicho ambayo ni haki yao kikatiba.

Akizungumza kwa simu na mwandishi, Kamanda Mwabulambo alikiri jeshi lake kuwashikilia katibu huyo wa Chadema wa kanda na mwenyekiti wa Bavicha mkoa lakini akasema yupo nje ya ofisi hivyo hawezi kulizungumzia jambo hilo kwa undani.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nasikia kutapika polisi wa Tanzania kuwa wana siasa

    ReplyDelete
  2. Nasikia kuharisha nikisikia hili neno uchochezi

    ReplyDelete
  3. Hii ni mara ya kwanza katika dunia kuona jinsi polisi wa nchi yetu walivyo na nguvu kuzidi Mungu. Kitu cha kushangaza zaidi, wanauwezo mkubwa kuwashika watuhumowa kwenye mitandao.lakini motandao hii hii kwa mika kumi na zaidi omeshindwa kuwakamata majambazi, mafisadi wamuu wa nchi hii waliotufikisha hapa ingawa vithibitisho benki vipo.kinachonishangaza zaidi, ni chadema kwa miaka kumi wamelia sana kuhusu ufisadi wa nchi hii na polosi ilishindwa muwakamata sababu sheria haikuruhusu.
    Sheria hizihizi. Zimeshindwa kumfikisha Raisi aliyepita mahakamani ingawa alimiri ana majina ya mafisadi na wauza unga. Wote wanashuria mushirikiana na polisi wote nchini wala hawakumgusa na kumuuliza kwa nini anawafuga ikiwa yeye ni mtawala wa ngazi za juu na amiri jeshi nchini.ni yeye aliwafuga mafidadi wakuu wote nchini kwa moaka mumi. Raisi wa sasa Mavufuli kwa kusikia milio ya Chadema na ukawa ndicho milochomfanya na kumtia nguvu atumbue. Leo kawageuzia mibao si Wanachadema, as Ukawa tu, yeyote anayedai haki ya demokrasi na kuwaziba midomo, muwanyanyasa, kuwapiga stop hata kufanya jambo lolote la kimaendeleo isipokuwa wana cm na yeye tu na polisi.
    Miongozi mkuu wa mkoa anapewa mamlaka ya juu sawa na raisi, kuwasulubu vyama vyote vya upinzani.ni nani na sheria ipi inampa hii nguvu potofu.wanaccm wamejitwalia sheria kononi muburuta watu wazima, mafasaha wanaozijua sheria za nchi na kuwaburuza mahakamani bila hata kupepesa macho.ni vijana hawa, wengine hata sheria za nchi hawazimudu sawasawa, jamani watu nchi nzima hasa ccm mnaounga nkono mamilioni ya watu hamzioni kama hizi ni vita vya ndani kwa ndani na hayaoni madhara kijamii, na hada uhasama unaojijenga , madhara ni makubwa sana sidhani kama mnayaona.waziwzi. yanangojea kutumbuka tu. Je mtawaua wote wanaotetea nambo hili, je mtawafungia mamilioni ya watanzania wote ambao hamkubaliani nao, je mtwafuata wote mitandaoni, kwenye emali kama mlivyoanza, manumbani, makanisani, misikitini? ,watanzania wanataka uhuru wa kuabudu, kuzungumza mutenda kazi ili taifa lisonge mbele. Taifa ni kweli lina wajinga wengi kama Makamba alivyosema, uwezo wakufikiri na elimu ya chin.elimu imeshuka kiwango kwa zaidi ya miaka mumi sasa ni haohao walitawala kwa kuachia elimu ishuke ndio wanaunga mkono.walikuwa busy kujimilikisha mali na juibia nchi, kutoa mikataba mibovu, munyan"ganya ardhi za watanzania na kusababisha migogoro ya ardhi nchi nzima. Leo badala ya kuwatumbua hao mnawaficha na kuwanyanyasa waliokuwa mstari mbele kumemea.mnawakumbatia ingozi wote waliosababisha haya na mnekataa kuwachukulia hatua na kuwapa kinga. Ni hao inabidi wachukuliwe hatua cha kushangaza na wao wapo kwenye utumbuaji je mnayemtumbua hapa ni nani kama mtumbuaji mkuu bado kakalia mali zote alizozichuma.si ndio hao wanaomuunga raisi wa sada, polisi, wanajeshi.ni hawa walitumika pia kulinda uharamia huu. Tanzania ni nchi ya amani kutokana na jinsi mwalimu nyerere alivyoweza kuikomboa nchi hii kwa amani bila kutoa damu.utashi ya kiongozi huyu baba wa taifa, hamuna kiongozi yeyote kwa sasa atakayediriki au kujifananisha naye. Ni utashi wa hali ya juu na imani binafsi. Kwrnda kanisani si swa na kuwa na utashi au imani.jwenda msikitini kila siku haimpi mtu utashi, wengi ni mazoea na siasa tupu.viongozi wengi wanapenda sifa, kuonekana, haya ni majanga matupu. Kiongozi mwenye hekima na utashi anatumia muda mwingi kimya kuomba, kutafakari atende haki, na si kupiga kelele na kumemea kila kukicha.kiongozi mwenye hekima na utashi kabla hajajitokeza hadharani atahakikisha kisheria anachokifanya kinaendana na sheria za nchi na kuhakimisha kila mtu ana uswa. Kumtendea mila mtanzania sawa na kumpa haki sawa, kumlinda sawa bila kujali cheo, kabila, jindia, dini au umri.kuna watu wanaabudiwa muzidi mungu, kunawatu wspo lamini hWaonekani wala hawawajali, hata wakiwapita hawana haja ya kujua matatizo yao sababu ni masmini, vilema, yatima, au wamevaa nguo chafu bila viatu. Au wako vijijini, hWapati haki zao.ndivyo mfumo huu unavyoelekea. Ni hatari kubwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hatari Si kubea Kama uunavyofikiria ila itaakuwa kubea Kama hatutowasgughulikia nyiyi mapotoshaji wenye Nia Na lengo la kuvuruga amani ya ncchi yetu..lengo lenu Na Nia yenu tunaielewa Na inaeleweka...kuwemi raia wema Na wazalendo msiburuzwe Na wachache wente masilahi binafsi

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad