Kauli ya Magufuli Yawachanganya ACT Wazalendo

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kauli ya Rais John Magufuli kuruhusu wabunge kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo yao pekee ni kukiua chama hicho.

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo, Bakari Licapo amemtaka Rais kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kauli hiyo ambayo alidai inahatarisha ustawi wa chama hicho.

“Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Mgwira alifanya kampeni nchi nzima ila kwa sasa atashindwa kuzungumza na wananchi wachache waliompa kura kutokana na kauli iliyotolewa,” amesema Licapo jana.

 Licapo, amewaomba vijana bila kujali itikadi, kutekeleza azimio lililotolewa na Zitto la kuandika barua zitakazotumwa Ikulu kueleza masikitiko yao juu ya ukandamizaji wa demokrasia.

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Semeni nyinyi tukisema
    Ukawa -:)

    ReplyDelete
  2. Kwani muda wakujinadi si bado? mbona wanatak kuvuja sheria bure? eh? Acha mambo yenu bwana.

    ReplyDelete
  3. Hivyo Azimio maana yake Ni nini?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad