HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, imelikataa ombi la kuiomba Mahakama hiyo iwapatie Kibali cha Kufungua mahakamani hapo ombi la kuomba Mahakama hiyo iifute amri /uamuzi wa Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu ya kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa nchini kwasababu ya dosari za kisheria .
Uamuzi huo ulitolewa Juzi na Jaji Kiongozi Fredinand Wambali wakati Katika ombi Na. 52/2016 lililowasilishwa Mbele yake na Baraza la Udhamini la Chadema lilokuwa kikitetewa na wakili wa kujitegemea Peter Kibatara dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Inspekta Jenerali wa Polisi waliokuwa wakitetewa na Mawakili wa serikali Haruna Matagane na Daniel Nyakeha.
Jaji Wambali alisema mlalamikaji alikuwa na Maombi mawili.Ombi la kwanza Chadema ilikuwa ikiomba Mahakama hiyo iwapatie Kibali cha Kufungua Kesi ya kupinga amri na uamuzi wa IGP wa Kuzuia mikutano na maandano ya vyama Vya siasa nchini na ombi la pili waliomba Mahakama hiyo itoe tamko la Kusema amri na uamuzi Huo wa IGP Si halali kisheria.
Uamuzi huo ulitolewa Juzi na Jaji Kiongozi Fredinand Wambali ambapo alisema amekubaliana mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi kwamba huwezi kuomba amri ya mapitio ya amri ya IGP Mahakamani hapo wakati mlalamikaji alikuwa na Mlango mwingine wa kupinga amri ya IGP na Mlango huo ni kwa mlalamikaji Kupenda kupinga amri ya IGP kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na alishindwa kufanya hivyo.
" Chadema walipaswa kukatia rufaa amri hiyo ya IGP ya Kuzuia maandamano ya vyama Vya siasa Kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na sio kwenda kushitaki mahakamani' alisema Jaji Wambali na hiyo ikapatikana Katika Kifungu Cha 43(6) sura 322 ya Mwaka 2002 ya Judicial Review .
Aidha Jaji Wambali alisema anakubaliana na pingamizi la pili la Mawakili wa serikali ambalo lilidai Kuwa ombi Hilo la Chadema litupwe kwasababu ombi Hilo la Chadema halikuambatanishwa na maelezo ya mlalamikaji na hayo maelezo yakidhi matakwa ya Kanuni ya 5(2) of The Judicial Reviews Rules of 2014 ambayo inataka hiyo hati ya mlalamikaji ifafanue maelezo na jina la mlalamikaji.
" Chadema Katika shauri Hili hayo yote walishindwa kuyafanya hivyo Mahakama hii inatupilia Mbali ombi Lao la kutaka Mahakama hii itamke amri ya IGP Kuzuia maandamano ni batiri kwa gharama kwasababu ombi la Mlalamikaji halijakidhi matakwa ya kisheria.
CHADEMA pia wameamuliwa kulipa gharama za kesi.
Lissu aibwaga serikali mahakamani kwenye habari ya Lissu na vilevile kichwa cha habari hii kama waandishi hamko bias mgeandika Serikali yaibwaga Chadema mahakamani tungewaelewa lakini habari za Chadema na Lissu mnazipamba kwa udi na uvumba ili waonekane jeuri
ReplyDelete