Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi wa haki za binadamu.
Aidha, Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi la Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa Mkoa.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a) vya Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya Sheria za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu au taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka ya madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.
Imetolewa na:
(SIGNED)
Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Agosti 26, 2016
Hili jipu lazima uma ulitumbueteba haraka
ReplyDeleteTulisena kuwapa vyeo watoto wadogo hii ndo faida yake
Anaropoka tu
Hivi Tanzania hakuna watu kuwafundisha viongozi jinsi ya kuongea kwenye media
Hata jinsi ya kukaa kwenye media?
Old is gold
Nafikiri huu utumbo wa haki za binadamu TANZANIA ni upuuzi wa hali ya juu
ReplyDeleteHivi ni nani aliruhusu huu upuuzi uwe established Tanzania??? Alifanya kosa kubwa sana
Watanzania ni malimbukeni hawakuhitaji huu upuuzi wa haki za binadamu kwani hawajui nini maana yake wala kazi zake kwani mwisho watadai watuhumiwa walevi wapelekewe bia Segerea au Keko
Hivi si CHADEMA hawa??? mbona wako sana kutetea wahalifu na wezi???? Sijasoma wakitetea walikatwa mishahara yao visivyo ila wakwenda sambamba na UKAWA au CHADEMA
Tanzania mhalifu auawe iwe kwa moto au vyovyote vile kisha haki za binadamu pigeni kelele au itabidi muwe victimised kwanza ndo mjue nini mnatetea maana mzigo alobeba mwenzil ni kama kifurushi cha pamba au siyo???
Mhalifu piga ua tu na ndio mwendo siyo kubembeleza MWISHO,, Mhalifu mvishe tairi kisha washa motooooo
Wewe mpumbavu na mjinga kama huyo unaye mtetea
DeleteTunaishi dunia ya uwazi na ukweli
Ukiona kiongozi hataki
Ushauri
Wala kukosolewa
Huyo ni dikteta tena uchwara
Au mpuga mapepe
Yaani chuya
Fyuuuuuu
ujinga mtupu
ReplyDelete