Nimepata taarifa ya mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Waandishi wa habari kuhusu kilichoitwa “wadaiwa sugu” wa NHC ambapo katika orodha hiyo kampuni ambayo nina hisa ya Mbowe Hotels Co.Ltd imeorodheshwa kama mdaiwa anayedaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni moja.
Nakiri kuwepo kwa mgogoro wa kibiashara wa miaka mingi baina ya Kampuni hii na NHC. Aidha kampuni hii imekuwa ikilipa kodi stahiki kwa NHC kwa mujibu wa makubaliano yetu ya kibiashara.
Kumekuwepo na ukakasi wa muda mrefu kuhusiana na mkataba wetu wa umiliki, uendelezaji na uendeshaji wa jengo hili unaochagizwa na msimamo wangu wa kisiasa.
Haki na Uhuru wetu wa kufanya biashara kama raia wengine umekuwa ukiingiliwa mara kwa mara katika mazingira yanayoambatana na Vitisho kiasi ambacho Maamuzi kadhaa hayafanyiki kwa hofu ya kisiasa kwamba “Itakuwa kumwongezea nguvu Mpinzani”. Hivyo, ningependa umma wa Watanzania uelewe kuwa sidaiwi na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC). Kufuatia utata huu wanasheria wa Kampuni wanashughulikia jambo hili kwa taratibu za kibiashara na kisheria.
Naomba kuweka wazi kwa yeyote anayehusika. Sitafungwa fikra, sitafungwa mdomo na sitaacha kuutetea Ukweli, Haki na Demokrasia katika nchi hii kwa misingi ya “kulinda kinachodhaniwa ni maslahi yangu ya kibiashara”. Wafanyabiashara wengi wanafungwa fikra na midomo ndani ya nchi hii kwa kuogopa hila na ghiliba za watawala.
Ni heri kufa masikini nikiwa nimesimamia ukweli, kuliko kuishi tajiri niliyetawaliwa na ubinafsi, woga, hofu na ubatili.
Natambua kuna jitihada za kutumia kila silaha na kila hila dhidi yetu katika Kipindi hiki.
Mwisho, Natoa rai kwa wanachama na wapenzi wa Haki katika Taifa hili, wasiogope. Haki itaweza kucheleweshwa kwa muda tu, lakini kamwe haiwezi kuzuiwa. Binadamu akikufungia mlango Mungu wa Haki atakufungulia dirisha.
Ubatili ni wa mpito lakini Haki ni ya milele.
Watatapatapa sana
ReplyDeleteTatizo lao ni vilaza wa kufikiri
Wamezoea vijembe, umbea, uzushi, uchochezi
Ndo hadi Leo hawajiamini
Lowassa na Sumaye wanatesa sana
Yote wivu tu Mbowe mwenyekiti wetu
Usiwe a Shaka
kilaza mkubwa kama anadaiwa si akalipe, vijembe na umbea viko wapi hapo wakati anatakiwa akalipe deni la NHC? na bado zile alizoficha China nazo mpaka zirudi, na huyo lowassa na mr. o wanatesa nini wakati wanakaa kwa wasi wasi ya kutufilisiwa?
DeleteKoma wewe huna Kazi
DeleteKazi kujitia kada wa CCM
Kusifia walipewa madaraka
Unafiki Magu atakupa cheo sahau mtabaki hivyo hivyo kuninyinia mitandaoni kujibu
Upunbavu na u
Umbea na kuhack wana CCM wenzenu waonekane wabaya
Wasikunyime usingizi
ReplyDeleteWenyewe kwa wenyewe hawaelewani
Leo wanaponda awamu ya nne ilyowaweka madarakani
Naaza kupata picha kwanini wametawala miaka zaidi ya 50 Tanzania
Hakuna maendeleo
Chama kimejaa wezi, waongo, wambea,
Wazuchi
Wameiba Mali zote za watanzania na kujitisisha lakini bado omba omba
Ukiwa mfanya biashara Upo upinzani shida Tanzania
Mungu ibariki Tanzania
Wanasiasa wetu bhana ni kiboko sasa Mbowe uachwe kushughulikiwa na kudaiwa kisa mwanasiasa ukidaiwa unasema njama kwa hiyo Mbowe tuthibitishie kuwa madai hayo ni ya uongo na hudaiwi sio blah blah
ReplyDeleteMungu ni mwema,na jee wangepewa nchi si tungenyonywa mpaka kope?wangegundua wafanyakazi hewa hawa kweli?wangelipa kodi?
DeleteWanakera na hawajiongezi.
Pumbavu wewe na wote wanakusapport
DeleteKwa lipi kwanza mmeiba agenda za ukawa Leo mnatamba
Na tunajuwa CCM wenyewe mnasaliti Magu
Kwani wengi wenu ni mafisadi papa
Namuonea huruma Magu bora angehamia ukawa ndoto yake ingefanikiwa
Wapinzani wanatumika na mataifa ya nje, tusipokuwa makini tunauana wenyewe kwa wenyewe
ReplyDeleteMdau, umesema, Hawa wapinzani wanatumika na mataifa ya nje yaliyoendelea tena Yale mataifa wasiopenda kuona bara hili la Africa likinyanyuka kwani hawapendi Kabisaa!!!! Wanapenda kuwaona wafrica wanatabika, wanangaika wanauwana, ili waendeleee kufaidika na Mali asilia wanazozipata katika bara hili, ndio maana kutwa kuwachochea wafrica, wakishaona kuona uongozi mzuri tu hawapendi, watawachochelea wale wajinga wajinga weee mpkaaa, Nayo hii inachangia bara hili kuporomoka, Kila siku siasa tu za ujinga ujinga, baadara ya kufanya kazi kwa maendeleo na mustakabali wa Taifa Bali ndio haya Kila siku, wakati huko kwao, Kuna muda wa siasa karibu na uchaguzi, ukishaa basi, iliyobaki ni kazi, tena kwa kushirikiana siasa mpka muda wake tena wa uchaguzi ukianza, lakini huku Kwetu Kila siku ndio hayo hayo, tuna matatizo sana sisi wafrica
DeleteAny.1.33 Pitia kwa mangi ukapate juice ya ukwaju.
DeleteNchi imeshaanza kuwa na adabu,tunafanya kazi,tunawahi kazini,kila mtu anaogopa rushwa nk.sasa badala ya kuendelea na HAPA KAZI TU eti tuendekeze siasa na maandamano yasio na tija.WATATUCHEKA.
Toa mikataba na vielelezo vyako,uone kama utafatwafatwa.
ReplyDeleteKwani mbona wengi wameipata pata kutoka NHC kutokana na sera ya HAPA KAZI TU ya awamu ya 5?
nikiwemo mimi mwenyewe sehamu yangu ya biashara?
ACHA VIJISABABU VYA KIS....
Senge wewe nini
DeleteHahahahah!Hiyo haimo Mbowe,na uache visingizio.KAWAJIBIKE.
ReplyDeleteunadaiwa bana na NHC, Hivi mchechu ni kichaa aongee na waandishi wa habari kuwa unadaiwa???? Mbowe acha siasa zako lipa deni hili ni shirika linalojiendehsa na fedha hizo za kodi.
ReplyDeleteHata hivyo umevumiliwa saana, lipa deni hacha porojo mbona wengine hawajatoka povu na ni taasisi za serikali.
acha bana kila kitu sio siasa, nyie ndio mnarudisha maendeleo ya nchi nyumba. lipa deni lako.
Ni kweli unadaiwa bhana na unatuangusha sana maana Uliapa kuwa kazi yako ni kuhuisha uzalendo,uadilifu,na awajibikaji katika uongozi wa nchi,KUIMARISHA AMANI,UMOJA NA MSHIMAMANO WA TAIFA ambao ndio msingi Mama wa kuleta maendeleo ya jamii TZ.Hapo je?kutolipa kodi ndio uadilifu?Mkuu umechemka>
ReplyDeleteHAPA KAZI TU INAHUSIKA NA SI VINGINEVYO.LIPA DENI NDIO DAWA,
ReplyDeleteNANI AMWAGE UNGA WAKE KWA KUKULINDA WEWE NA MADENI YA MUDA MREFU?
hata kama una deni..kula..lala..kwani kuwa na deni imeanza kwa MBOWE?Serikali zenyewe zinadaiwa..hakuna news hapo..msituchoshe.
ReplyDeleteDENI SI LINAONEKANA?KAMA UMELIPA ONYESHA USHAHIDI.
ReplyDeleteKwa fikra umefungwa babu,labda mdomo ndio hujafungwa.
ReplyDeleteKitendo cha kupanga maandamano 01/09/2016 alhamisi siku ya kazi ni kufungwa fikra,yaani hata kama maandamano yangekuwa kihalali.
MASKINI MBOWE!DAAAAAAAAAAAAH
ReplyDeleteYAANI JAMANI MPAKA NAMKUMBUKA DK.SLAA.
Yeah,TZ kwanza Mbowe baadae,
ReplyDeletelipa deni watu tupate mikopo tutakaporudi vyuoni babangu eeh.
Pumbavu nyote na ofisi za serikali nazo zifungwe
DeleteMbowe haami Kama mnategea kukodi pale CCM
Mmeula na chuya kapigeni disco Msoga au Chato
Kelele zote hizo Mbowe kumbe unayako mengi uliyoyaficha. Sasa nenda tu kalipe madeni kabla ujaumbuliwa zaidi. Majipu mengi yamejificha Chadema sijui hao wanaowaunga mkono hawana macho au akili......
ReplyDeleteKwa hii awamu ya tano dawa ni kulipa tu.Hakuna ukanjanja.
ReplyDelete