Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Joyce Ndalichako .
“Kutokana na mambo yaliyobainika serikali imechukua hatua ikiwemo kuvitaka vyuo vikuu vilivyopokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku Saba kuanzia leo, ” amesema.
Amesema vyuo vinatakiwa kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za akaunti za benki ambazo fedha za mikopo hulipwa ili kuondoa udanganyifu.
“Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa zote za wanafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili,” amesema
NDIO ZIRUDISHWE HARAKA SANA
ReplyDeleteKimenuka
ReplyDeleteHuu ndio uadilifu tunao utaka na kuuona.. Ujanja Ujanja hatuupendi... Kula kimisheni town kusitishwe tuna taka nguvu jasho. Unakula kwa kazi yako na si ki hewa Hewa.. Baba Magu na sisi wote tunalikataa hilo!! Hongera mama Ndalichako Kazi yako ni Nzuri na Tunaipenda... Tena warudishe haraka Sana
ReplyDelete