Usiku wa August 7 2016 Ligi Kuu Ubelgiji iliendelea tena kwa klabu ya KAA Gent kuikaribisha KRC Genk katika uwanja wa GHELAMCO wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000 ili kucheza mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Ubelgiji.
Katika dakika zote 90 KRC Genk walicheza na kumiliki mpira kwa asilimia 40 wakati wenyeji wao KAA Gent walikuwa wameutawala mchezo kwa asilimia 60, licha ya KRC Genk kufanya mabadiliko katika safu ya ushambuliaji kwa kumtoa Nikolaos Karelis na kumuingiza mtanzania Mbwana Samatta dakika ya 66, walifungwa goli 1-0.
KRC Genk kutokana na kuwa ugenini na kushambuliwa kwa kiasi kikubwa, hali ilikuwa mbaya dakika ya 90 baada ya KAA Gent kupata goli la ushindi na kujichukulia point tatu kupitia kwa mshambuliaji wao aliyeibuka mfungaji bora msimu uliopita Jeremy Perbet, Genk itacheza nyumbani August 13 2016 dhidi ya W. Bevern.