Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini amemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuwa Arusha tumejiandaa vyema kwa ajili ya Operesheni UKUTA, na kwamba Mwigulu siyo wa kwanza duniani kutoa lugha za vitisho duniani. Lema amesema kuwa tumejiandaa kufa ama kuuawa na Jeshi la Polisi wakipigania haki na kuikumbusha serikali kuacha kuvunja katiba ya nchi ambayo Rais na viongozi wote waliapa kuilinda.
Mh Lema ameyasema hayo kumjibu Mwigulu Nchemba aliyesema anawaonya chadema wasitingishe kiberiti, kwamba viberiti vingine vimejaa gesi.
Lema amesema kuwa kauli za hovyo zinazotolewa na serikali zinaweza kuingiza nchi kwenye machafuko. Amesema Farao Mungu alimfanya moyo wake uwe mgumu ili Apate kujitukuza mbele ya wana Israel, na kinachoonekana hivi sasa ni kwamba Mungu ameufanya moyo wa Magufuli kuwa mgumu ili Tanzania ili iweze kukombolewa.
Lema amesema kuwa hatumjaribu mtu bali wakati wa kuandamana bali tunatetea utawala wa sheria uzingatiwe, tutaandamana kutetea haki yetu ya kikatiba kufanya mikutano.
Amesema kwamba kwa sababu wamejiandaa kutupiga, nasi tumejiandaa kwa kila kitu, kwamba tunajua tarehe moja siyo siku ya harusi, kwamba tarehe moja tumejiandaa kwenda jela ama kuawa.
Tunajua tunakwenda kukumbana na polisi wakiwa na silaha na mabomu lakini tumejiandaa.
Kama Mauti imepoteza utukufu wake kwangu, hakuna statement yoyote inayoweza kurudisha Arusha kuandamana.
Amemuonya Mwigulu apime kauli zake kabla hajaitoa.
Lema amesema madai ya chadema ni madai ya msingi na endapo madai yake yatapuuzwa nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.
Mh Lema amesema hatuandamani bei ya konyagi ipungue, bali tunaandamana utawala wa sheria katika taifa hili uzingatiwe.
Kama leo haturuhusiwi kufanya mikutano ya hadhara kwasababu rais amesema, iko siku misikitini ama makanisani itafungwa kwasababu rais amesema. Hii vita ni ya kila mtu katika taifa hili, siyo vita ya chadema
Nitakuja kumalizia baadaye kidogo nimalizie natafuta namna ya kuiweka clip hapa
Lema Amjibu Waziri Mwigulu. Asema Yupo Tayari Kufa Akipigania Haki Operation Ukuta
7
August 22, 2016
Tags
MIMI SIMO WALA SITHUBUTU.
ReplyDeleteHamuishiwi sababu?
ReplyDeleteHivi kiongozi wako kuhimiza tuache siasa na tufanye kazi imekuwa nongwa,mnabadilisha maneno ili mradi tu msikike?Kweli kwamba nyie wenzetu hamuoni juhudi za rais?Kusema ukweli mimi ni mpinzani lakini siwaelewi kabisa nyie ndugu,kila kitu mnakosoa kwani kuna binadamu asiye na kasoro?SUA tupo tunawasubiri mje kama hamtakiona cha moto,na ni vizuri mkatangulia wasemaji wakuu sio kuwatanguliza walala hoi wenzetu.Mtatulazimisha mpaka tuwakosee adabu msiopenda amani wakubwa nyie.MNACHOSHA KWA KWELI AAAH!
Msenge wee
DeleteUsiojuwa kuchamba wala kutawaza
Wapinzani bi chachu ya maendeleo dunia nzima
Acheni ushamba CCM
Miaka 50 mmefanya nini Tanzania ?
Na siku mkishika dola mtatengeza dictionary
Deleteza matusi,sasa hapo kwa nini umemtukana?kwani si
kachangia anachokiona,au yeye sio mtanzania?
Miaka 50 kulikuwa na mafisadi ndio walioharibu akiwemo hao mnaowakumbatia huko chadema,na sio kwamba hakuna maendeleo ila kwa kuwa wewe na kundi lako lengo
ni kuponda kila la ccm mnajifanya hamuoni,mtakufa mmoja baada ya mmoja kwa kihoro cha kukosa madaraka.Mlaaniwe!
Huko ndio kufa kwa upinzani kwani sasa hawana hoja ila kilichobaki ni kuwahamasisha wapuuzi wenzao ati kuingia mitaani ati kupinga udikteta ambao hata wengi wa hao waandamanaji hawajui
ReplyDeleteHivi Dikteta huchaguliwa???
Chadema si wajinga hivyo kwani wameona kasi ya Magufuli itauwa upinzani kabisa ndio maana wamekuja na mpango wa kuleta vurugu ili kumchafulia
Kuwepo mpango wa kuwaelimisha watu juu ya nia ya CHADEMA
Ndugu yangu sio kulaumu Tuombe Mungu yasitokee. Tuepushe kauli yoyote ya kumuudhi mtu. Likitokea litaniumiza maana nina ndugu kila kona ya nchi hii hata wale wanaotaka kuandamana ni ndugu zangu pia wanaowaambia wasiandamane ni ndugu zangu sasa naomba kwa MUngu kisiwepo kuandamana wala kuzuia kutikisa kiberiti.
ReplyDeleteGodbless Lema wewe ni mwanaume kati ya wanaume wachache waliopo nchini,Mungu akutunze na akujalie maisha marefu na mwisho mwema
ReplyDelete