Lembeli Aibuka Mkutano wa Rais Magufuli

Mbunge wa zamani wa jimbo la Kahama, James Lembeli aliyehamia Chadema ameibuka leo katika mkutano wa na Rais John Magufuli uliofanyika mjini Kahama.

Akihutubia wananchi wa Kahama, Rais Magufuli amemkaribisha Lembeli na kumtaka kurudi  CCM akisema kwa Tanzania anayoijua yeye hatakuwa amepoteza mkia, kwani huko aliko ndiko mafisadi wamekimbilia.

Hivi karibuni akihutubia mkutano Mkuu wa CCM, Rais Magufuli akizungumzia waliotoka kwenye chama na kurejea tena, alitoa mfano wa ng’ombe aliyekatwa mkia, akisema huwezi kumzuia kurejea zizini lakini wenzake wanamkua kuwa hana mkia.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lembeli amesema amekwenda kwenye mkutano huo kwa kuwa kazi anayoifanya Rais Magufuli ndiyo ambayo alikuwa anapigania wakati akiwa

mbunge kwa kuwa Shinyanga rushwa ilikuwa imekithiri.

Amesema na  hawezi kurudi CCM mpaka Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho akisafishe.

"Kubadilisha msikiti siyo kuacha Uislamu, nyumba itaposafishika nitarudi," amesema Lembeli.

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SAFI,HAPO NI KUSEMA WAMEANZA KUELEWA MAANA YA HAPA KAZI TU NA KWAMBA SIASA SIO UADUI.LEMBELI ANAJUA KABISA JPJM ATASAFISHA CCM,HAYO ALIYOYASEMA NI MANENO YA AKIBA TU KWAMBA KESHO MTASIKIA KARUDI CCM.

    ReplyDelete
  2. Na Lowasa atarudi CCM.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama atarudi Naamini ni fisadi na anatafuta msamaha bila kutumbuliwa. ingependa kujua ukweli wa mambo kati ya Lowasa na Kikwete. Kuna kitu hawa wawili bado hawajakiweka hadharani. Na kama Lowasa anarudi CCM kuna makubaliono kati ya hawa wawili kuzimisha kabisa utumbuaji. Hapa Watanzania ndio watakaoumia. Chanzo kikuu cha Ufisadi kieanzia kwa Mkapa wakati Lowasa akiwa waziri mkuu. Akaja Kikwete akamtoa. Kunasiri kubwa iko hapa hawakukubaliana madili fulani. Sasa yanazikwa watakuwa marafiki tena chini ya Magufuli na kikwete endapo atarudi.Siasa ni hatari kubwa. Watanzania lazima wawe waangalifu na wadadisi badala ya kufurahia. Namwona pia Zito Kabwe kauli inbadilika baada ya kuwa tajiri. Wote hawa wataififisha hoja ya ufisadi na imeshaanza kufifia kiasi fulani. Sasa lawama yote inamlenga Mboye, na CHadema. Watanzania kweli ni rahisi kufunikwa shuka .

      Delete
  3. kuacha msikiti sio kuacha uisilamu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kuhangaika na kujitafutia maslahi binafsi. Huna ubunifu wako binafsi kujiingizia pesa unategemea sisa. Hapa ni cheo ndani ya Magufuli unakutafuta baada ya Lowassa kutochaguliwa. Naona hakuna maslahi. huu si uzalendo bali ubabaishaji wa maisha kibinafsi ili uingie kwenye nguvu kipesa.

      Delete
  4. Hawa Ni viongozi pia wasio na msimamo pekee. Wanaotegemea maslahi yao kutoka chama tawala kama Augustino Mrema. Sacrifice, hawana. Subira, hawana. Wanatafuta vyeo ndani ya chama ili kumudu maisha yao. Na utasikia tu. akirudi atapata cheo. Huu si uzalendo tunaouzungumzia. Mzalendo ni yule mtu hayumbi. Sasa naona wengi waliotoka na wengine wanamakosa yao kwa kujirudisha CCM ni kupata kinga ya maovi yao bila kuchukuliwa hatua yoyote. Wote wanaoridi, wengi wanaomsifia hawatatumbuliwa hata. Raisi ataangalia upande na hatawagusa. Tatizo ni moja, Mbona huendelei kutumbua kama ulivyoanza. Bandarini bado, Kwenye gesi bado, kwenye ardhi za wamasai na nguzo kuu za uchumi zilivyozawadwa kwa Wageni bado, kwenye waua tembo na Watoroshaji wanyama bado, waliotoa vibali vya kuwinda bado, Kwenye ESCROW bado, Kwa wauza unga wakuu bado,kwenye Katiba bado.Nakupongeza machache uliyoyafanya. Lakini kila hotuba nakusikia kuwa mimi ndiye Raisi, mimi ndiye mwenyekiti wa CCM hakuna umodest bali mimi. Kwa watu wanaoshangilia bila kuelewa hii mimi bosi nawashangaa. Ni wewe peke yako MMmm. Hakuna sisi ambayo nchi yetu imejengwa kwa namna hii . Inatisha mtu mmoja Kiongozi haoni hii mimi, mimi, mimi ni Tatizo badala ya sisi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad