Lowassa Atoa Waraka Kuhusu Kukamatwa Kwake

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa waraka akisema kitendo cha askari wa Jeshi la Polisi kuwakamata wakati wakiwa kwenye kikao cha ndani cha Chadema jana  kimemuimarisha na kumpa nguvu zaidi ya kudai demokrasia.

Katika waraka wake kwa vyombo vya habari leo, Lowassa amesema anafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi Watanzania walivyoipokea operesheni yao ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) iliyopangwa kuanza kesho kwa maandamano na mikutano, lakini vitendo vya polisi vinawapa wasiwasi wananchi.

Lowassa, akiwa na Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, John Mnyika (naibu katibu mkuu-Bara) na viongozi wengine wa chama hicho kikuu cha upinzani walikamatwa jana wakiwa kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Hoteli ya Girrafe na baadaye kwenda kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano kabla ya kuachiwa na kutakiwa kwenda kituo hapo kesho.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera mzee wetu
    Africa hakuna demokrasia
    Ukihamia upinzani tu umekuwa jaidi,
    Mchochezi, Mhaini
    Asante wala usife moyo tupo nawe
    Tutakukumbuka maishani
    Kama Martin ruther King
    Wa Tanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. huna lolote

      Delete
    2. Makubwa!Sio huyu aliitwa fisadi papa na nyie haohao?ila sasa
      kwa kuwa yuko chadema unamfananisha na Martin Ruther?UWIIIIIIIIIIIIIII

      Delete
    3. Watoto wa haramu utawajuwa tu
      Pumbavu nyinyi mama zenu kuranda Dodoma mkazaliwa
      Nyinyi baba zenu ndo hii mijizi
      Kwa miaka 53
      Fyuuuuuuuuu

      Delete
  2. HUYO MARTIN ALIKUWA FISADI KWANI?

    ReplyDelete
    Replies
    1. huyu mzee namshauri siasa za majukwaani kwake zimepitwa apumzike .maana atadhalilishwa hata dola hawezi kupata .chadema vigeugeu kesho watamwita msalit

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad