MABASI ya Dar Mbeya, Mwanza Sasa Kuchukua Siku Mbili Njiani Badala ya Siku Moja..

Waliozoea kusafiri kwa mabasi kwa siku moja kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya na kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza na kwingineko kwenye umbali sawa na huo, sasa inabidi wajipange kisaikolojia kutumia siku mbili kukamilisha safari hizo. Hayo yamebainishwa na Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geofrey Silanda. Uamuzi huo umetokana na utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo na kubaini kwamba mabasi yanayofanya safari kwenye mikoa hiyo hayapaswi kusafiri kwa siku moja.

Toa maoni yako
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapana hii sio sawa kwakweli,....

    ReplyDelete
  2. Kwa vile Wao wanapanda ndege ndo maana wanatuwekea maamuzi mabovu,

    ReplyDelete
  3. Sawa km ni swali la usalama ni dhahiri basi likitumia mwendo halali barabarani haliwezi lifikie liendapo (Mwz, Musoma, Kigoma, Bukoba, n.k) ndani ya masaa yanayoruhusiwa kusafirisha abiria barabarani. Ila chakufanya hapo kibusara kwa SUMATRA ni kwanza kupima kila basi la liendalo mbali na madereva yake kwa kuhakikisha usalama upo wa kutosha, cha pili ikiridhika mamlaka kutoa kibali maalum cha usafirishaji nje ya masaa ya kawaida ili hayo mabasi na abiria yake yaweze kuanzisha safari zao mapema zaidi (k.mf saa tisa, kumi) na kufikia yaendapo kwa mda halali. Kwani SUMATRA pia ni wakala watoaji huduma kwa dola na raia wake na sio tu mamlaka ya kuamulia sheria na masharti mapya bila kuzingatia matokeo yao na hati za raia!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad