Madiwani wa Ukawa wa Manispaa ya Kinondoni wamesusa kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kiongozi huyo hana uhusiano mzuri na viongozi wa upinzani.
Jana, Makonda aliitisha kikao cha wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara za manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na madiwani wote, wakiwamo wabunge wanaounda halmashauri hizo.
Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Arnaoutoglou kililenga kuzungumzia masuala mbalimbali, kama maeneo yaliyovamiwa na uboreshaji wa elimu mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema Makonda amekuwa na tabia ya kudharau na kutoheshimu viongozi wenzake, hasa wa upinzani akiwaona hawatendi kazi vizuri.
Pia, Jacob alidai kuwa Makonda amekuwa na tabia ya kuingilia kazi zinazofanywa na viongozi wengine kwa kutumia cheo cha ukuu wa mkoa, jambo ambalo meya huyo alisema ni kinyume cha sheria.
“Akitaka tumpe ushirikiano, Makonda abadilike la sivyo mtindo utakuwa huuhuu, mambo yatakuwa hivi. Huu ni mwanzo na ndiyo maana leo (jana) Ukawa Kinondoni tumekuwa na msimamo mmoja,” alisema Jacob.
Jacob, ambaye pia ni diwani wa Ubungo (Chadema), alisema hawakuona umuhimu wa kwenda katika kikao hicho kwa sababu kiongozi wa mkutano huo anawadharau.
Akijibu tuhuma hizo, Makonda alisema madiwani waliohudhuria kikao hicho maeneo yao yalikuwa na shida na yanahitaji kushughulikiwa, hivyo si kazi yake kuhesabu watu na kubaini nani hakufika mkutanoni.
Alisema ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana namna bora ya kuvirudisha viwanja vilivyochukuliwa na kuvirejesha kwa matumizi yaliyokusudiwa.
“Huyo anayelalamika mwambie huo anaoufanya ni utoto akikua ataacha. Narudia tena siyo kazi yangu kuangalia nani hajaja kwenye kikao,” alisema.
Kwenye kikao hicho, meya wa Ilala (Chadema), Charles Kuyeko alikuwapo kwenye mkutano huo pamoja na madiwani wenzake, sambamba na wale wa Temeke.
Makonda si mgeni wa tuhuma .Aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kionondoni katika kipindi ambacho alikuwa akituhumiwa kuhusika kwenye sakata la kupigwa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba kwenye mdahalo wa Katiba uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl.
Katika kipindi hicho, Makonda pia alikuwa akituhumiwa kumrushia tuhuma za ufisadi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiahidi kuwa CCM isingempitisha kugombea urais.
Akitoa majumuhisho ya kikao cha jana kilichoanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi, Makonda aliwataka watu waliovamiwa na kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, kuanza kubomoa majengo yao kabla ya Serikali kuwafikia.
Kabla ya kutoa majumuisho hayo, Makonda alitoa nafasi kwa madiwani wa manispaa hizo kueleza kero zinazowakabili, hususan zinazohusu ardhi.
“Najua mchakato huu utawagusa hadi vigogo, lakini mimi siogopi vita kwa sababu ndani yangu ninaongozwa na Mungu pekee,” alisema Makonda.
Mbali na hilo, Makonda alisema endapo mtendaji wa ardhi atayebainika kuhusika katika kuchezea michoro na ramani ili aachie ardhi na kujipatia fedha, atashughulikiwa kwa mujibu sheria.
Katika hatua nyingine, Makonda amemwagiza kamishna msaidizi wa ardhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mathew Nhange kumwambia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi awaondoe maofisa ardhi na mipango miji wa Kinondoni na Ilala baada ya kushindwa kutoa taarifa za kuridhisha katika mkutano huo.
Huku akiwataja maofisa hao wanaotoka Kinondoni na Ilala, Makonda alisema alishakutana na wakuu wa idara kwenye vikao vilivyopita, hivyo alitegemea kuwa watumishi hao wangetoa taarifa zilizokamilika.
“Kamishna naomba umwambie katibu mkuu mimi siwataki watumishi hawa katika manispaa hizi. Mwambie awatoe na kuwapangia kazi nyingine,” alisema Makonda.
Kamishna Nhange alisema agizo hilo analifanyia kazi na kwamba atampa katibu mkuu taarifa za watumishi hao jana.
Si anatumwa na wakunwa wake
ReplyDeleteYale Yale naibu spika
Nashangaa Kama mnafanya kazi vizuri
Kwanini wawe waogope wapinzani ?
Nyie viongozi wetu wa Kinondoni mnatushangaza sana sisi wana wa nchi. mnasema Mkuu wa Mkoa anawadharau! mlisha kutana naye lini tena? hii ilikuwa ndiyo fursa maridhawa ya kueleza kero zenu siyo kulalamika kwenye mitandao,haitawasaidia. acheni ushabiki wa vyama vyenu hapa sisi tunataka mpange na kutekeleza maendeleo ya wilaya yetu. Mstahiki wewe ni kijana una bahati kuwa kwenye Mkoa na Wilaya zinazoongozwa na vijana, usiogope kukutana nao na 'kuwachallenge'kwa hoja siyo kususiasusia wananchi tunataka kuyakimbilia maendeleo kwenye Wilaya yetu, acheni hizo..
ReplyDeleteNini cha ajabu hapo?? Hao chadema kususa susa kama wanawake ndio kawaida yao....HAKUNA JIPYA, WAJARIBU KUJA KIVINGINE. Mheshimiwa PMakonda, piga kazi baba, waache wasuse, wakisusa wengine twala.........HAPA KAZI TU
ReplyDeleteAKILI ZENU MBOVU SANA,HAMJUI KUSUSIA MNATUUMIZA WANANCHI TULIOWACHAGUA?
ReplyDeleteKomeni nyinyi
ReplyDeleteMnalazima watu watutushe
Makonda it's not people choice
Sisi tunawakisha watu waliotuchaguwa
Tunajuwa mnaona aibu mji mkuu kongozwa na ukawa
Kwa mnaleta chokicho
Lakini yote wivu
Mji yote ukawa si madc si RC wote ni against ukawa
Fyuuuuuuuuu
Agombane na mashoga wenziwe
ReplyDeleteWanamjuwa kichwa hadi Miguu
Atuwache madiwani