Kesho yake mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliongea na Amplifaya ya CloudsFM pamoja na millardayo.com na kuthibitisha kwamba mwimbaji huyu amekubali mwenyewe kwa hiari yake na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu ya kuachana na dawa za kulevya huko Bagamoyo Pwani.
Sasa leo Agosti 6, 2016 tumepata taarifa nyingine kwamba staa huyo kahamishwa kutoka Sober House ya Bagamoyo na kuhamishiwa Sober House ya wanawake tu walioathirika na madawa ya kulevya iliyopo Kigamboni.
Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV mmiliki wa kituo hicho Nuru kayaongea haya..
Mimi naitwa Nuru ni mmiliki wa Sober House ya wanawake tu iliyopo Kigambo juzi tulipata ugeni kutoka kwa Msanii Ray C alikuja kuomba matibabu kwasasa yuko anaendelea vizuri na amekubaliana na hali yake’- Nuru
‘Tumempokea vizuri na yeye mwenyewe amefarijika sana kiufupi tu mashabiki wake wamuombee dua sana na mpaka sasa hivi afya yake inaendelea vizuri’- Nuru
" Mashabiki wake wamuombee dua sana" Mtu wa kumuombea ninani. Anayepaswa kuombewa labda ni mtoto mdogo yeye kama anataka akajiombee mwenyewe. Chagua moja kifo au maisha.
ReplyDelete