Makamba: Adui wa nne nchini ni usawa kati ya walionacho na wasionacho

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba amesema tangu nchi ipate uhuru miaka 50 iliyopita, maadui watatu ambao ni maradhi, umaskini na ujinga wapo pale pale lakini kuna adui wa nne aliyeongezeka.

makamba

Ameyasema hayo Ijumaa hii jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua ripoti ya hali ya kipato cha uchumi Afrika Mashariki iliyotolewa na Taasisi ya Society for International and Development (SID).

Alimtaja adui huyo kuwa ni tofauti kubwa ya usawa kati ya walichonacho na wasichonacho.

“Katika safari ya nchi yetu tumepata wazungu wapya ambao ni Waafrika wenzetu. Watu wanaishi maisha mazuri sana, watoto wao wanapata elimu nzuri sana, sasa hivi tofauti imekuwa ni kubwa sana,” alitoa mfano huo Makamba.

“Kama nchi inataka kujenga taifa la watu walio sawa hakuna budi kukabiliana na suala hilo, kwani usawa katika fursa ndiyo nyenzo muhimu ya kukabiliana na usawa katika jamii,” aliongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. The same old song"wote waliotangulia maybe kabla hata ya wewe haujazaliwa waliimba wimbo huo huo wa maradhi umasikini elimu na ujinga wameondoka lakini hali ndiyo ikazidi kuwa mbaya sasa umekuja wewe unaimba wimbo huo huo waliouimba wenzako hapo zamani bahati nzuri sasa hivi wabongo wana upeo wa kuona mbali sana kwa hiyo huo wimbo wako sidhani kama kuna mbongo ambaye atausikiliza shauri wimbo huo umeisha-expire long time wewe kaa kwenye hiyo position uliyopewa ujinufaishe wewe familia na marafiki zako husijifanye kuwa una uchungu sana na wabongo wasio kuwa na uwezo/kitu kuwa wewe/nyinyi wanasiasa eti mtakuja kuwakomboa ki hali au kimaisha wabongo walio dhoofu ful hali

    ReplyDelete
  2. Wewe Makamba na familia yako au ukoo wako mpo upande gani kati ya adui wa nne. Nyiyi wanasiasa zungumzeni maneno yenu matamu lakini ukweli utabaki palepale wengi wenu sio wa kweli, mnashibisha matumbo yenu na familia zenu ila Mungu yupo tutaishia kusikiliza porojo zenu. PS Mpaka sasa mwanasiasa anayejali watu katika Tanzania ni Rais JPM. Wengine walio wengi kama wewe Makamba na wenzako ni maneno matupu. Nakutakia siku njema.
    JB. USA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad