Makonda Kuwajengea BAKWATA Ofisi ya Kisasa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi ramani ya jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ikiwa ni ahadi ya kuwajengea jengo hilo.

Akizungumza wakati akikabidhi ramani hiyo, Makonda alisema jengo hilo linatarajiwa kuwa na ghorofa tatu na litagharimu zaidi ya Sh bilioni tano.

“Ijumaa nitakuja hapa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi na niseme tu ujenzi utaanza hivi karibuni na nimeshawaambia watu wangu wahakikishe jengo hilo linajengwa kwa muda usiozidi miezi 14 tu,” alisema Makonda.

Licha ya kukabidhi ramani hiyo, Makonda pia aliwataka viongozi hao wa dini kuendelea kuhubiri amani ili taifa liendelee kuwa na amani na mshikamano. Alisema ujenzi wa jengo hilo, umekuja baada ya kuona kuwa Bakwata imekuwa na mchango mkubwa kwa taifa ikiwemo kuhubiri amani na mshikamano.

“Viongozi wa dini ni watu muhimu sana wamekuwa wakituhubiria amani na pia viongozi hao wamekuwa wakituongoza katika safari ya kutupeleka kwa mola, endeleeni kudumisha na kuihubiri amani ili taifa ili liendelee kusifika,” alisema Makonda.

Kwa upande wake, Mufti wa Tanzania, Shehe Mkuu Abubakar bin Zubeir alimshukuru Makonda kwa uamuzi alioufanya; na kusema ameonesha njia kwa wadau wengine walio na wasio waislamu kujitolea kuchangia.

“Najua jamii inaweza kushangaa kwa nini nimepokea msaada kutoka kwa mtu ambaye si Muislamu, lakini niseme tu hata Mtume alipokea misaada kutoka kwa watu kama hawa, ni rai yangu kuwaombeni na ninyi Waislamu mjitokeze kuunga mkoa juhudi hizi kwa hali na mali,” alisema.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yetu macho
    Msaada billion 5
    Toka kwa Makonda?
    Haya tutaona mengi na kusikia mengi
    Lakini watanzania tunajuwa mchele na pumba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani hata tupayuke vipi kwa mabaya au mazuri tunayoona kiukweli haisaidii kwa watanzania walio wengi,wameweka nta masikioni.Watanzania wanachotaka ni amani tu basi hata kama mtoto anakaa chini darasani,hata kama maji hakuna n.k wenyewe hawajali.Ukitaka kupima angalia commentS za watu kwenye jambo la kipuuzi kuliko la siasa hasa kukemea CCM.MUNGU NA ATUSAIDIE,TUTAVUKA TU.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad