Ndani ya miaka nane na zaidi wananchi tumeimbishwa na kuaminishwa usiku na mchana kuwa Lowasa ni Fisadi mkubwa wa uchumi wa Tanzania.
Na mbaya zaidi mkasema mnaushaidi wa ufisadi wa Lowassa kama anabisha aende mahakamani.
Wengi tuliamini na mpaka sasa tumesimama kwenye misingi ya uaminifu kuhusu Chadema kuwa Lowasa ni Fisadi na hafai kupewa nchi.
Lakini wengi wetu mmeshindwa kutushawishi kwa hoja kwa nini Lowassa awe msafi sasa.
Ni vema mtuombe radhi hadharani kuwa ndani hiyo miaka mlikuwa mnatudanganya na kutulaghai ili kuwalaghai na ccm wamteme Lowassa.
Bado nipo kwenye misingi ya awali ya Chadema kupinga ufisadi na mafisadi na naamini Lowassa ni fisadi mpaka pale viongozi wa Chadema mtakapokiri wazi kuwa mlitupotosha Lowassa sio fisadi na ushahidi mlikuwa hamna.
Mbowe na CHADEMA, Lini Mtatuomba Radhi Watanzania Kuwa Mlidanganya Lowassa sio Fisadi
11
August 01, 2016
Tags
Hawawezi kuomba radhi hawa ni wasanii tu, wako kimaslahi zaidi kuliko kutetea wanyonge. Hapo ni tonge nyama tu
ReplyDeleteKoma wewe
DeleteKuna ufisadi kama ccm
Lembeni kasema wapi mbele ya Magu
Wasanii mafilauni waliokufisha na umbumbu huu ambao ata maji ya kuoga pumbavu kushabikia ujinga.
DeleteCCM ilianza wakati Raisi kikwete alipomweka hadharani Huyu kuwa fisadi na mpaka leo anaendelea kufanya hivyo Mbona hamjamuuliza.
ReplyDeleteKikwete mpaka leo amesema Chadema ndiko walikokimbilia mafisadi. Mbona hamuulizi. Raisi Kikwete kaikalia listi ya Wauza unga wakuu na mafisadi wakuu kaiacha nchi njia panda iliyojaa ufisadi mkuu ambao JMP anatumbua wote mmekaa kimya na cha ajabu hata Ras=isi wa sasa hajamuuliza nipe hiyo list ya watu niifanyie kazi lakini hajaiomba.
Naona Watanzania wengi hamna msimamo huru na msimamo kamili. Mnaruhusiwa kuyumbishwa na chama mpaka mtakapotumbukia tena. Kwa nini msimuulize Mzee slaa moja kwa moja. yeye ndiye alikuwa na majarada. Itakuwa rahisi kwake kwani sasa hayupo ndani ya Chadema. Watanzania ni rahisi kusahau mambo na nani amefuga mafisadi kwa miaka ishirini. Ni hiyo hiyo CCM na viongozi toka ngazi za Uraisi mpaka chini. Kama si wao hakuna cha kutumbua. Mbona mnageuza kauli. Mbona Hamjamuuliza Raisi aliyepita ilikuwaje ukawafuga mafisadi List unayo je? Ni fikra kama hizi bila kukata kiini cha matatizo kwa sababu zisizojulikana, badala yake kufumba macho na kuwaminya wanaojaribu kuleta uhuru, maendeleo na kutoa ufisadi. Kama Watanzania mnakubali kumuuliza Raisi moja kwa moja na kumtaka aadhibiwe bali wote mpo njia moja kufuga ufisadi au nanyi mpo kwenye kundi hili la ufisadi na kutokutaka kutumbuliwa. Na kama mna nia na mnamuunga Magufuli na kumsapoti asilimia miamoja hamtakwenda mbali bali kumuuliza Raisi moja kwa moja raisi aliyepita kuruhusu ufisadi chini yake na kuficha majina yao kwanza. Ni yeye chini ya himaya yake haya mafisadi yameibuka na kutanda kila kona. Nawangojeeni mtakapokuwa tayari kufanya hli, msifumbe macho watu, midomo na masikio hapa. Nitawaona shujaa na mna nia.
Hao ni wababaishaji saana achana nao?
ReplyDeleteWewe huna jipya kama wenzako, kuleta uhuru upi ambao hatuna, acha jazba wakati wa kuchangia hoja. Jiulizeni Lowasa ni fusadi au siyo fisadi? kama siyo aeleze ukwasi alionao aliupataje na biashara ipi?nashanga pia kusikia mtu kama ww unauliza list yawauza unga wapo wapi ama kapewa nani? jibu unalo nani muuza unga unayemuona nje kwa sasa. Tatizo kuna kuendekeza uwanaharakati badala ya siasana ukweli wa mambo. Je unafahamu kuwa kumeanzishwa mahakama ya mafisadi? au ulikuwa nje ya nchi? kwa ufupi siasa kwenu zimefikia tamati.
ReplyDeleteUsijikoshr na kutetra mambo ambayo inabidi yafanyiwe kazi. Jibu swali. Orodha iko wapi. Staight forwad.mnazoea kukingia viongozi vifua. Najua mahakama ipoinaanza. Lakini swali linajirudi palepale alete orodha aliyoikumbatia akiwa raisi wa nchi hii.msipotoshe umma.unajua nyinyi watu badala ya kuongea ukweli, kutenda haki kwa wote mnaleta majibu mkato. Haya mambo ndiyo yatakayosafisha nchi na kuleta amani, usawa na sheria safi na sawa kwa kila mtanzania. Acheni ufinyu wa kufikiri.
DeleteKuwa njr ya nchi ai ndani .kila dskika internet ipo.hii si tatizo. Tatizo no ukweli wa mambo uliopo.na swali la Lowasa si chadema tu.lilanzishwa na raisi aliyepita na bado limeebdelea kwenye mkutano mkuu wa ccm.na kama ni fisadi kwa nini hakuchukuliwa hatua yeyote.kama mnamhitaji arudi mrudisheni.kikao cha kusaka uraisi alikataliwa na ccm sababu hizo.kila kitu kipo mtandaoni. Au hamtaki kufuatilia ukweli.yangu kikazi yanakuhusu yanaingiaje hapo.mefuata soku nyingi najua.
DeleteTunasubiri familia ya mboe ianze kuandamana ndo na cc tufuate
ReplyDeleteTeh teh teh!hata mimi nitakuwa nachunguliachungulia nikiwaona wako kwenye maanadamano nafunga tela.
DeleteMbowe alifikiri kwa kuahirisha UKUTA angesamehewa deni la NHC. Kumbe wapi! Jamaa wamwmkomalia. Ninavyoandika sasa, vifaa vya ofisi na vyombo mbalimbali vinatupwa nje, OMG.
ReplyDelete